Habari za Punde

Wziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Afungua Kitengo Cha Kuchuja Damu Katika Hospitali ya Bombo Mkoani Tanga.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifungua kitengo cha kuchuja damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa  wa Tanga ya Bombo, Machi 1, 2020.  Wa tatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Mwita Waitara na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua kitengo cha kuchuja damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo, Machi 1, 2020. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela,  wa tatu kulia ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa pili kulia ni Mganga Mfawidhi  wa hospitali hiyo, Dkt. Naima Yusuf
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Christopher Nyange mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika  kitengo cha kuchuja damu baada ya kufungua kitengo hicho katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mganga ya Bombo, Machi  1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.