Habari za Punde

Wananchi wa Zanzibar Wakiwa Katika Harakati za Maandalizi ya Sikukuu ya Eid Fitry Wakijipatia Hahitaji Yao Wakizingatia Kujikinga na Maambukizi ya Corona

Askari wa Baraza la Manispa Zanzibar wakiwapima joto Wananchi wanaoingia katika Marikiti Kuu ya Darajani kwa kupata mahitaji mbalimbali katika marikiti hiyo.Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja umechukua tahadhari kwa wananchi wanaofika katika marikiti hiyo kupimwa joto la mwili kuepusha maambukizi ya maradhi ya Corona na kutakiwa kuvyaa barkoa wanapoingia katika eneo hilo.
Askari wa Baraza la Manispa Zanzibar akimpima Mwananchi Joto la mwili wakati wa kuingia katika Marikiti Kuu ya Darajani Zanzibar kujipatia mahitaji ya bidhaa mbalimbali  
Wananchi wakinawa mikono kwa maji ya kutiririka na sabuni kabla ya kuingia katika Marikiti Kuu ya Darajani Jijini Zanzibar. ikiwa ni zoezi la kujikinga na maambukizo ya Corona.
Mfanyabiasha ya tungule (nyanya) akiwa katika marikiti kuu darajani akisubiri wateja wa bidhaa hiyo. Kilo moja leo imeuzwa shs.1500/=  
Wananchi wa Zanzibar wakipata hahitaji yao ya bidhaa kwa ajili ya maandalizi ya kusherehekea Sikukuu inayotarajiwa kufanyika kesho kwa kuandama kwa mwezi baada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mjasairiamali wa bidhaa za majumbani akiwa katika eneo la marikiti kuu ya darajani akiwa amezingatia maelekezo ya Wataalam wa Afya kuvya barkoa  katika maeneo ya mkusanyiko wa wnanchi kama alivyokutwa na camera yatu ya zanzinews. katika eneo la marikiti hiyo akisubiri wateja wa bidhaa hizo mbuzi ya kukunia nazi. nyungo, miko na bidhaa nyegine.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.