Habari za Punde

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ( ZSSF) Yakabidhi Msaada Kwa Kituo cha Watoto Yatima na Nyumba ya Wazee Sebleni Zanzibar.

 
Afisa Uhusiano Mkuu wa Masoko Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Mussa Yussuf akimkabidhi Msaada wa vyakula na vifaa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Corona kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizni, akipokea msaada huo Mkuu wa Kituo cha Watoto Mazizini Bi.Sharifa   

Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF  umetoa msaada wa chakula na vifaa mabalimbali wenye thamani ya shilingi milioni 16 kwa  wazee pamoja na watoto yatima.
Akikabidhi msaada huo Afisa Uhusiano Mkuu na Masoko (ZSSF) Ndg.Mussa Yussuf amesema 
“ZSSF imekuwa na desturi ya kutoa msaada kwa wazee na watoto yatima kila mwaka ili kuwafariji na kuunga mkono juhudi za Serikali’’
Miongoni mwa vitu vilivyotolewa ni pamoja na ndoo, vitakasa mikono, unga wa ngano, sukari, mafuta ya kupikia, barakoa na nguo kwaajili ya wazee wa kituo cha Sebleni.
Aidha msaada huo umetolewa kwa wezee wa kituo cha Sebleni na kituo cha watoto yatima Mazizini .Nae Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii Bi.Wahida Maabadi ameushukuru uongozi wa ZSSF kwa kutoa msaada huo na kusema
 “Msaada huu umekuja wakati muafaka tukiwa tunaendelea kupambana na janga la corona na utasaidia kwa kiasi kikubwa” amesema
Mkurugenzi Ustawi wa Jamii Bi. Wahida Mabaad akitowa shukrani kwa Uongozi wa ZSSF kwa msaada wa huo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Watoto Yatima Mazizni Jijini Zanzibar na kushoto Afisa Uhusiano Mkuu na Masoko ZSSF Ndg. Mussa Yussuf. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizni Jijini Zanzibar. 
Baadhi ya Vyakula na Vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Corona vilivyotolewa na ZSSF kwa Wazee wa Sebleni na Watoto wa Mazizini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.