Habari za Punde

Viongozi Tawi la CCM Muembemajogoo Kutumia Vikao Halali Kuondosha Migogoro.

Na.Takdir Suweid - Zanzibar.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mgharibi Bw.Mgeni Mussa Haji amewataka Viongozi wa Tawi la  ccm Muembemajoo kutumia vikao halali kuwaondosha Madarakani wanaokwenda kinyume na Maadili ya Chama hicho ili kuondosha mizozo inayoweza kujitokeza.
Ameyasema hayo huko Muembemajoo Wilaya ya Mgharibi ‘’B’’ wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Tawi la Ccm Utajiju.
Amesema kama kuna Viongozi au Wanachama wanaokwenda kinyume na Maadili katika Tawi hilo wanapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa taratibu za Chama na sio matakwa yao binafsi.
Aidha Katibu Mgeni, amekemea baadhi ya Wanachama wa Chama hicho wanaotangaza nia ya kugombea na kuanza kupiga kampeni kabla ya muda uliopangwa na kuahidi kukatwa majina yao watakapoomba ridhaa ya kuongoza.
 Hata hivyo amewashihi Viongozi wa Majimbo kushirikiana katika kuwatumikia Wananchi bila ya Ubaguzi ikiwa ni kutekeleza Ilani ya Chama hicho ya mwaka 2015-2020.
Nao Viongozi wa Tawi hilo wamesema tatizo kubwa linalowakabili ni pamoja na Makundi,Ubaguzi na uroho wa Madaraka kwa baadhi ya Viongozi jambo ambalo linaondosha ufanisi wa kazi zao na kuwaomba Viongozi wa Mkoa huo kuingilia kati ili kuondosha matatizo hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.