Habari za Punde

WAJUMBE WA KAMATI YA MAAFA YA WILAYA KASKAZINI B WAPEWA DOZI YA SHERIA ZA KUKABILIANA NA MAAFA

Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Kaskazini B ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasazini B Rajab Ali Rajab akifungua Kikao cha mafunzo ya Sheria ya Kukabiliana na Maafa kwa Wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Wilaya  Kaskazini B   pamoja na Kamati ya Kitaalamu (kulia) Mkurugenzi wa  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar  Makame Khatib Makame na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya kaskazini B ,Mwanajuma Pembe
Wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Wilaya  pamoja na Kamati ya Kitaalamu ya Kukabiliana  na Maafa ya Wilaya Kaskazini B  wakisikiliza mafunzo ya kukabiliana na maafa kwa Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na  Maafa  Zanzibar Makame Khatib Makame  (hayupo pichani )  huko katika Ukumbi wa  CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja..
Picha Na Khadija Khamis - Maelezo Zanzibar.

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar  18/06/2020
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Kaskazini B ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Rajab Ali Rajab amesema  kuwepo mipango mikakati ya kukabiliana n maafa kutasaidia kuepusha athari katika jamii.

aliyasema hayo huko Ukumbi wa  CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja. Wakati akifungua mafunzo ya Sheria ya Kukabiliana na Maafa kwa Wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Kaskazini B  pamoja na Kamati ya Kitaalamu ya kukabiliana na Maafa ya Wilaya hiyo.

Alisema  kuwa yakitokea maafa Wajumbe wa kamati washirikiane kwa pamoja kuyapatia ufumbuzi kwa haraka ili kupunguza athari zitakazojitokeza katika janga hilo.

Hata hivyo aliishauri kamisheni ya maafa kuendeleza kutoa elimu ya masuala ya maafa ili kujenga uelewa katika utekelezaji wa majukumu kwa wajumbe .

Nae Mkurugenzi wa  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar  Makame Khatib Makame aliwafahamisha wajumbe
kutekeleza majukumu yao ili kutimiza lengo lililokusudiwa.

Aidha ameitaka kamati ya kitaalamu kuwashauri wajumbe wa kamati  ya maafa Wilaya kwa lengo la kupunguza athari za maafa .

Vile vile amesema kamati hizo zikae vikao vya mara kwa mara ili kuitayarisha mipango na miongozo itayofanya kazi litapotokea janga la maafa.

Kwa upande wake  Afisa Mawasiliano na Tahadhari Omar Ali Mohamed alisema kamati ielewe dhana ya maafa na kukabiliana nayo  ili kuirudisha hali ya baadae.  

Akitoa ufafanuzi wa  kukabiliana na maafa kwa  Wajumbe hao alisema ni kuanzisha  mfumo wa mawasiliano pamoja na kutayarisha ramani itayowaonyesha maeneo hatarishi kwa wilaya .

Aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kutoa elimu kwa wananchi na njia sahihi ya kujiepusha na maafa ili kuepusha athari zitakazotokea.

Alisisitiza kuwa wajumbe wawe na utaratibu wa kufanya tathmini ya mwenendo mzima wa majukumu yao ili kazi  zifanyike kwa ufanisi .

Nae mwanasheria wa kamisheni ya kukabiliana na maafa Thureya Ghalib alieleza sheria ambazo zinatakiwa kufuatwa na wajumbe hao pamoja na utaratibu wa kiutendaji.

Alifahamisha kuwa katika sheria ya maafa kuna makosa ya adhabu kwa yeyote atakaekataa kutekeleza majukumu yake bila ya sababu atakuwa kafanya kosa kisheria .

Nae ASF. Asha Othman Saidi wa kutoka Kikosi cha Zimamoto Zanzibar ameeleza changamoto walizonazo ni pamoja na jamii kutoa taarifa zisizosahihi za tukio la Maafa.

Alieleza kuwa miundo mbinu ya ujenzi  katika maeneo mbali mbali ni miongoni mwa changamoto zinazojitokeza katika kazi zao.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.