Habari za Punde

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ,Dkt Charles Kimei akirejesha fomu za kuwania Ubunge Jimbo la Vunjo  ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,anayepokea fomu ni Katibu wa CCM wilaya ya Moshi ,Miriam Kaaya .
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi ,Miriam Kaaya akipitia fomu za Dkt Kimei mara baada ya kuzipokea .
Watia ni wa nafasi za Ubunge katika majimbo ya Moshi vijijini na Vunjo ,Victor na Dkt Charles kimei wakioneshana jambo kwenye simu wakati walipokutana katika ofisi za wilaya ya Moshi kwa ajili ya kuchukua na kurejesha fomu .

Na Dixon Busagaga ,Moshi .
JUMLA ya Makada 473 wa chama cha Mapinduzi wamejitokeza kuwania nafasi ya Ubunge katika majimbo ya mkoa wa Kilimanjaro kupitia kura za maoni huku kati yao 99 ni wale wanaomba nafasi kupitia viti maalumu .

Zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi limeendelea huku ikishuhudiwa baadhi ya Makada wakifika katika ofisi za wilaya ya Moshi vijijini kwa lengo la kuchukua fomu hizo.

Miongoni mwa waliorejesha fomu ni pamoja aliyekuwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt Charles Kimei aliyechukua fomu ya kuwania Ubunge katika jimbo la Vunjo ambapo alirejesha fomu yake katika ofisi za CCM wilaya ya Moshi na kupokelewa na katibu wake Miriam Kaaya .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.