Habari za Punde

TCRA Yawataka Mafundi wa Simu Zanzibar Kuwa na Mikataba na Wateja Wao Kuondosha Malalamiko Yasio ya Lazima

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar Bi. Esuvatie-Aisa Masinga akizungumza na Mafundi wa Simu za Mkononi Zanzibar, wakati akifungua Semina ya Siku moja kwa Mafunzi wa Simu Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.    
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar Bi. Esuvatie-Aisa Masinga akisisitiza jambo wakati wa Semina ya Siku moja kwa mafundi simu za mikononi Zanzibar na kuwataka kufanya kazi zao kwa ueledi, semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.   
Mafunzi wa Simu za mkononi Zanzibar wakifuatila hutuba ya ufunguzi wa Semina ya Siku moja kwa Mafundi Simu ilioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar wakati Mkuu wa TCRA Ofisi ya Zanzibar Bi.Esuvatie-Aisa Masinga (hayupo pichani) akizungumza katika semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Eng. Mtende Hassan akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Semina ya Siku Moja ya Mafundi wa simu za mkononi Zanzibar ilioandaliwa na TCRA Ofisi ya Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdlwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Eng. Baluhye Kadaya kutoka TCRA Makamo Makuu Jijini Dar es Salaam akiwasilisha Mada wakati wa Semina ya Simu moja kwa Mafunzi wa Simu za Mkononi Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar. 
Mafunzi wa Simu za mkononi Zanzibar wakifuatila Mada ikiwasilishwa na Eng.Baluhye Kadaya, kutoka Makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es Salaam, wakati wa semina hiyo ya Simu moja kuwajengea Uwezo Mafundi  Simui za Mkonani Zanzibar, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.  
Mafunzi wa Simu za mkononi Zanzibar wakifuatila Mada ikiwasilishwa na Eng.Baluhye Kadaya, kutoka Makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es Salaam, wakati wa semina hiyo ya Simu moja kuwajengea Uwezo Mafundi  Simui za Mkonani Zanzibar, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.  
Mafunzi wa Simu za mkononi Zanzibar wakifuatila Mada ikiwasilishwa na Eng.Baluhye Kadaya, kutoka Makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es Salaam, wakati wa semina hiyo ya Simu moja kuwajengea Uwezo Mafundi  Simui za Mkonani Zanzibar, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.  
Mafunzi wa Simu za mkononi Zanzibar wakifuatila maelezo katika kabrasha za TCRA , wakati wa Semina ya Siku moja ilioandaliwa kwa ajili yao na TCRA Ofisi ya Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.


NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ofisi ya Zanzibar Esuvatie-Aisa Masinga amesema kukua kwa  uchumi wa Kati Tanzania umechangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta ya mawasiliano kupitia mafundi simu.

Hayo aliyaeleza alipofunguwa semina ya siku moja kwa mafundi simu wa Zanzibar iliyoandaliwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania huko katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni mjini hapa.

Alisema kuwa kila kitu ambacho kimepata mafanikio kuna hatua mbali mbali zimepitia ambazo zinakuwa fursa adhimu kwake.

Hata hivyo alisema kuwa mamlaka yao ina dira yake ambayo ni itaweza kufikia kiwango chenye hadhi ya kimataifa na kwa hali hiyo wameona na wao ni muhimu katika kufikia huko.

Kwa upande wake Mhandisi wa Mawasiliano kutoka TCRA Makao Makuu na fundi simu wa zamani Mhandisi Baluhiye Kadaya amesema kuwa teknolojia ya simu za mkononi imekuwa baada ya kila mmoja kubaini fursa zilizomo ndani yake.

Alisema kuwa sasa hivi kuna matumizi makubwa ya simu kuliko vitu nyengine vya electronic kutokana na urahisi wake kwenye matumizi.

Hivyo aliwataka mafundi hao kujaribu kulinda kazi hiyo na kutokuwa tayari kuruhusu wachache kuwaharibia.

Alisema kuwa ni lazima watu waelewe kuwa kazi hiyo inalipa, hivyo inahitaji kulindwa ili isiharibiwe.

Sambamba na hayo aliwataka mafundi hao kubadilika na kujaribu kuwa na mikataba na wateja wao ili kuondosha malalamiko yasiokuwa ya lazima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.