Habari za Punde

KAMPENI YA TANESCO YA MATUMIZI BORA NA SAHIHI YA UMEME YAHAMIA MKOANI GEITA

Na mwandishi wetu, Geita.              
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kupitia idara ya masoko, limeendelea  na kampeni yake ya kutoa  elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa migodi  na wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka safari hii mkoani Geita.

Migodi iliyotembelewa na kikosi kazi hicho cha TANESCO ni pamoja na Migodi ya Geita mjini, Wilaya za  Nyanghwale na Bukombe, lakini pia mashine za posho mills zilizotembelewa ni za Buseresere Kasamwa, Nyanghwale,Bukombe, Katoro na Geita mjini.

Kwa mujibu wa Eng Ally Koya kutoka kitengo cha masoko Tanesco makao makuu alisema lengo hasa la kampeni hiyo ni kuwawezesha kufahamu  jinsi ya kupunguza gharama ambazo si za lazima kwa kununua vifaa vya kisasa  na kuachana na vifaa vilivyochakaa na vya zamani kwani vinatumia umeme mwingi.

Wamiliki hao walielimishwa kuhusu utaraibu wa kufunga motor za kisasa na kuzifanyia service mara kwa Mara ili motor iendelee kuwa na ufanisi.

“Matumizi bora na sahihi ya umeme ni muhimu kwa usalama kwani umeme  ni nzuri kama ukiutumia kwa kuzingatia usalama lakini pia umeme ni moto mara moja.” Alisema Mhandisi………….

Walipewa pia elimu ya kufunga power factor ili iweze kuwasaidia uendeshaji wa mitambo yaani kVA haitakuwa kubwa.

Aidha wamiliki wa migodi na mashine walishukuru ujio wa wataalamu hao wa TANESCO kwani umewaongezea uelewa na hivyo kuongeza ufanisi katika eneo la matumizi sahihi ya nishati hiyo ya umeme.Wafanyakazi wa mgodi wakipewa elimu ya usalama
Fundi wa  mgodi wa genge tatu extech alishauriwa anaposuka motor asisuke zaidi ya mara mbili
Afisa uhusiano na huduma kwa wateja mkoa wa Geita akiandika changamoto wanazozipata hapo mashineni

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.