Habari za Punde

Mradi wa Tree of Hope Yahamasisha Uwajibikaji wa Matumizi ya Rasilimali za Umma Sekta ya Elimu


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Ndg.Charles
Mwaitega akipokea msaada mmoja ya Vifaa mbalimbali zikiwemo Ndoo na Sabuni  kwa ajali ya matumizi ya Hospitali na Vituo vya Afya Wilaya ya Handeni kutoka kwa Mratibu wa Mradi wa Tree of Hope Ndg. Goodluck Malilo (kushoto) hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,Ndg.Charles Mwaitega akipokea msaada wa vitakasa mikono na ndoo  27 na sabauni kwa ajili ya kunawia mikono katika hospitali na vituo vya afya vya Wilayani Handeni vyote vikiwa na thamani ya shs milioni 
7.5, ilivyotolewa na Tasasi ya Tree Of Hope. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tree Of Hope,Fortunata Manyeresi.

Na Hamida Kamchalla, HANDENI, TANGA.
Wajumbe wa Kamati za kuhamasisha uwajibikaji wa matumizi ya raslimaliza umma (SAM) sekta ya elimu zilizoundwa katika Vijiji vya Wilayani hapa,wameombwa kuihamisha jamii kushiriki ujenzi wa vyoo na madarasa yaliyokuwa yamesimama kwa sababu ya Covid 19.

Hatua hiyo imekuja baada ya ujenzi wa matundu ya vyoo,madarasa na nyumba za walimu kushindwa kukamilishwa kwa Wakati kufuatia  mlipuko wa Corona na hivyo kusababisha uhaba mkubwa wa miundombinu hiyo katika shule mbalimbali za Wilayani Handeni.

Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Tree Of Hope,Fortunata Manyeresi alitoa ombi hilo jana alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Kamati za kuhamasisha uwajibikaji wa matumizi ya raslimali za umma sekta ya elimu kutoka vijiji nane vilivyopo Wilayani hapa.

Alisema ukiwa ni mwanzo wa awamu nyingine ya  mradi unaoendeshwa na Tree of Hope kwa ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society (FCS) uhamasishaji wa uwajibikaji wa matumizi ya umma ,angependa kuona hadi ifikapo Disemba mwaka huu,majengo yaliyokuwa yamekwama kuendelezwa kwa sababu ya mlipuko wa Corona yanakamilishwa ili wanafunzi wapate elimu iliyo bora.

"Wajumbe wa Kamati hizi mnalo jukumu kuhakikisha mnatumia nafasi zenu kuwahamasisha viongozi na jamii ili ziweze kushiriki kukamilisha madarasa,vyoo na nyumba za walimu zilizokwama ziweze kuendelezwa hadi kukamilika" alisema Manyeresi.

Awali wajumbe wa Kamati za  (SAM) sekta ya elimu wa vijiji nane Wilayani hapa walisema mbali ya Corona kukwamisha ujenzi wa majengo na vyoo vya shule katika baadhi ya vijiji ilichangiwa pia na kukosekana uwazi na ushirikishwaji wa wazazi juu ya matumizi ya fedha zilizopelekwa na Serikali ,wadau au kuchangwa na wananchi.

"Wazazi na wananchi katika baadhi ya vijiji wamegoma kuchangia ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vyoo kwa sababu hawajui walizichangishwa awali, hawasomewa taarifa za matumizi yake na hata kwingine hawajajenga mbao za matangazo na hata zilizopo hazibandikwi taarifa" alisema Hamid Hussein wa kijiji cha Majani Mapana Wilayani hapa.

Mratibu wa miradi wa asasi hiyo,Goodluck Malilo alisema jukumu la wajumbe wa Kamati za SAM ni kuhamasisha uwazi,ushirikishwaji na uwajibikaji miongoni kwa viongozi na wananchi ili kuamsha ari ya kuchangia ujenzi wa miundombinu hatimaye ipatikane elimu bora.

Alivitaja vijiji vilivyo katika mradi huo kuwa ni Majanimapana,Kabuku nje,Hoza,Michungwani,Kitumbi,Mkata Mashariki, Kwedizinga na Msocha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.