Mkuu wa Zantel- Zanzibar, Mohammed Mussa akizungumza na wadau mbalimbali wakati Kampuni hiyo ilipoingia makubaliano na Kampuni ya Vigor Group wamiliki wa boti za ZanFast Ferries ili kuwawezesha wateja kununua tiketi kirahisi zaidi kwa njia ya Ezypesa.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Vigor Group, Abdallah Turky na baadhi ya watendaji kutoka Kampuni hizo mbili.Hatua hiyo inatarajia kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wasafiri wa ndani na nje.
Mkuu wa Masoko na Huduma za Kifedha wa Zantel, Sakyi Opoku akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Rahisi Solutions, Abdirahman Hassan baada ya Kampuni hizo kuingia ubia ili kuboresha huduma za mawasiliano kwa kuwawezesha wateja kununua tiketi rahisi zaidi kwa Ezypesa.Huduma hiyo ni ya kwanza nchini kutoka Zantel.Kulia ni Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Mussa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Vigor Group, Abdalkah Turky akizungumza na wadau mbalimbali wakati kampuni hiyo ilipoingia makubaliano na Kampuni ya mawasiliano ya Zantel ili kuwawezesha wateja wake kununua tiketi kwa njia ya Ezypesa.Kulia ni Mkuu wa Zantel Zanzibar-Mohammed Mussa na Kaimu Afisa wa fedha Zantel, Aziz Ali.
Wateja
waZantel wataweza kununua tiketi za usafiri wa boti za ZanFast Ferries
kwa urahisi zaidi kwa kulipa kwa Ezypesa baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na
Kampuni ya usafirishaji ya Vigor Group ambayo inamiliki boti za ZanFast Ferries
ili kuboresha huduma za ukataji tiketi kwa wateja wao.
Kampuni hiyo ni moja ya watoa
huduma za usafiri wa majini kati ya Zanzibar na Dar es Salaam zinazochangia
katika urahisishaji wa huduma za usafiri kwa wenyeji na wageni.
Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa
Zantel-Zanzibar, Mohammed Mussa alisema hatua hiyo imelenga kurahisisha
upatikanaji wa huduma za ukataji tiketi kwa abiria hivyo kuboresha maisha ya
wateja wao.
“Kwa kupitia Ezypesa
tunahakikaisha wateja wanafanya malipo yao kwa urahisi zaidi,mahali popote na
wakati wowote.Ushirikiano wetu naZanFast Ferries unawapa wateja uhuru zaidi wa
kununua tiketi na kupunguza muda na mchakato wa kununua tiketi,” alisema Mussa.
Ili kupata tiketi, mteja wa Zantel
atatakiwa kupakua application ya ZanFast Ferries kishanenda Kata tiketi,chagua
Ezypesa na fanya malipo.Baada ya kukamilisha malipo mteja atapokea ujumbe mfupi
(SMS) Pamoja na tiketi laini (e-ticket)
itakayotumika siku ya safari.
“Tunaamini
njia hii ni suluhu ya muda mrefu na itaboresha namna wateja wanavyopata huduma
za usafiri hususan wasafiri wa ndani kwani kwa sasa hakuna haja ya kwenda tena
katika ofisi bali ukiwa na simu yako tu unaweza kujihakikishai uhakika wa
kupata usafiri,” alisema Mkuu wa Masoko na Huduma za Kifedha wa Zantel, Sakyi
Opoku.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Vigor Group, Abdallah Turky alisema kampuni hiyo imejidhatiti katika kuboresha
huduma za usafiri kwa kuhakikisha inawapa wateja njia rahisi na za kidigitali
za kufanya malipo ya tiketi.
“Ushirikiano baina yetu na Ezypesa umetanua wigo wa njia za malipo sanjari
na App yetu ya ZanFast Ferries ambazo zinampa mteja uhuru wa kununua tiketi
mahali popote alipo,” alisema.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Zantel katika
kuleta huduma na bidhaa za kidigitali ili kurahisisha malipo kwa wateja wake.
Wateja watakaofanya malipo kwa Ezypesa watatumia tiketi laini (e-ticket)
badala ya tiketi za kawaida na watatakiwa kuwa nayo siku ya safari.
Kuhusu Zantel
Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano
Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya
mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.
Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa
huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya
Watu wa Zanzibar (PBZ).
Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za
intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic
cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na
duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa
nchini.
Aidha,Miundombinu hiyo imeiwezesha Zantel kutoa huduma za kimataifa
za sauti na data kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo kuchagiza
ukuaji wa teknolojia ya digitali.
No comments:
Post a Comment