Habari za Punde

Uzinduzi wa Mikutano ya Kampeni Katika Majimbo Mbalimbali ya Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Mjini Kichama Ndg.Talib Ali Talib, (kushoto) akimnadi mgombea Uwakilishi jimbo la Mwara, kupitia CCM Ndg. Mihayo Juma Nhunga, wakati wa mkutano wa uzinduzi  wa Kampeni ya Jimbo la Mwera zilizofanyika kiwanja cha Masingini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Mjini Kichama Ndg.Talib Ali Talib, (kushoto) akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwara Zanzibar kupitia CCM Ndg. Zahoro Mohammed Haji, wakati wa uzinduzi mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Masingini.
Mjumbe wac Kamati Kuu ya CCM Mhe. Zuberi Ali Maulid akimtambulisha Mgombea Ubuge Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Hamad Yussuf Masauni, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Kikwajuni uliofanyika katika uwanja wa mnazi mmoja.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kikwajuni Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Nassor Salim Aljazeera akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Kikkwajuni wakati wa mkutano wa kampeni wa jimbo hilo uliofanyika katika uwanja wa mnazi mmoja. 
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM )Bi. Tabia Maulid Mwita akimtambulisha Mgombe Uwakilishi kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndg. Ali Suleiman Mrembo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo uliofanyika katika uwanja wa kwarara .
Mgombea Ubunge Jimbo la Pangawe Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndg.Haji Amour Haji, akiinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, baada ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Maulid Mwita, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Pangawe Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Kwarara  
 (Picha na Abdalla Omar )


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.