Habari za Punde

Kongamano la Dua Maalum la Kuiombea Zanzibar Amani.

Kamati ya Amani ya Kitaifa ya Viongozi wa Dini Zanzibar inapenda kuwatangazia kuwaalika Wananchi wa Zanzibar kushiriki katika Dua Maalum ya Kuiombea Nchi ili kuendelea kubaki na Amani.

Kongamano huilo la dua litafanyika kesho katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Unguja

Kamati itafanya  Kongamano kubwa la kuiombea Nchi yetu ili iendelee kubaki na kudumu katika hali ya Amani,Utulivu na Umoja miongoni mwetu kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Oktoba,28, 2020.,

Wananchi Wote tunaombwa kuhudhuria katika Kongamano hilo kwa wingi kumuomba Mwenyenzi Mungu kwa lengo la kuiombea  Nchi Yetu Salama pamoja kila mmoja wetu.

Pia kumuomba Mwenyenzi Mungu kututatulia shida zetu mbalimbali zinazotukabili, Wanazuoni wakubwa kutoka ndani na nje ya Nchi watakuwepo katika Kongamano hilo maalum la dua.

    Shughuli hiyo itafanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu SUZA Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Kongamano litaaza asubuhi. 


AHSANTENI SANA NA NYOTE MNAKARIBISHWA, MUNGU IBARIKI ZANZIBAR, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA NA DUNIA KWA UJUMLA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.