Habari za Punde

MAPOKEZI YA MAJIRIBIO YA MELI MV.AMANI ZIWA TANGANYIKA KIGOMA LEO #JUMAPILI
 TAARIFA KWA WANA HABARI LEO SIKU YA JUMAPILI KUANZIA SAA 6 MCHANA NI MAPOKEZI YA MAJARIBIO YA MELI KUBWA ZIWA TANGANYIKA  MV.AMANI AMBAYO ITAWASILI BANDARI YA KIGOMA*


*Mv.AMANI ni Meli Kubwa katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika Kesho itawasili kwa Majaribio katika Bandari ya KIGOMA Ziwa Tanganyika lengo ni Kumuunga RAIS MAGUFULI katika Kufungua Fursa za Kiuchumi katika Mkoa wa KIGOMA pia na Nchi ya CONGO ,na Nchi zinazunguka Ziwa Tanganyika Kibiashara zaidi* 

*Uwezo wake wakubeba abiria zaidi ya 600,vyumba zaidi ya 22 vya Kulala vyenye ubora na kisasa , Uwezo wa Kubeba Mizigo zaidi ya Tani elfu 3500,Magari kubeba zaidi ya 50,inaenda kwa spidi ya haraka ndiyo Meli Kubwa Katika Ziwa Tanganyika ndiyo pekee kwa Majaribio ya Kwanza Kuja Kigoma katika Kumuunga Mkono RAIS MAGUFULI  kwa vitendo katika Kuimarisha Biashara katika Ya Tanzania ,CONGO pamoja na Burundi na Nchi zinazunguka Ziwa Tanganyika katika Kukuza Uchumi zaidi katika biashara katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika ambao walikuwa wanaouhitaji wa Meli za Mizigo na Abiria*


*Leo Itapokelewa kwa Majaribio ya Kwanza katika Mkoa wa KIGOMA na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh.Thobias Andengenye Majira ya saa 6 Mchana.Wananchi wote Mnakaribishwa wa Mkoa wa Kigoma*. 

*Imetolewa na*
     *Rock Mwakibinga Jr*
         *Afisa Habari na              Mahusiano*
(MV AMANI) 0629  999998
24/10/2020.
*Kigoma*

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.