Habari za Punde

Rais Dkt. Magufuli atoa pole kwa Familia ya Marehemu Briton Wilfred Mollel aliyeuwawa Tunduma mkoani Songwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kuwapa pole Familia ya Marehemu Briton Wilfred Mollel (26) Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM aliyeuwawa tarehe 25 Agosti 2020 Tunduma mkoani Songwe, kulia ni Mama Mzazi wa Marehemu Roda Bryson Mwaisongole akiwa pamoja na mke wa Marehemu Salome Philemon Mayao.  Tunduma mkoani Songwe leo tarehe 02 Oktoba 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi rambirambi yake ya Sh. Milioni 3 Mama Mzazi wa MarehemuBriton Wilfred Mollel, Roda Bryson Mwaisongole Tunduma mkoani Songwe ili ziwasaidie katika kipindihikikigumu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali pamoja na Familia ya Marehemu Briton Wilfred Mollel, kulia ni Mama Mzazi wa Marehemu Roda Bryson Mwaisongole, mke wa Marehemu Salome PhilemonMayao pamoja na Watoto wake wawili. Marehemu Briton aliuwawatarehe 25 Agosti, 2020 Tundumamkoani Songwe na ameacha Watoto watatu. Marehemu Briton alikuwa Mkuu wa Mafunzo na Mkuu wa Itifaki UVCCM Wilaya Momba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.