Habari za Punde

Uzinduzi wa Barabara ya Fuoni Hadi Kombeni Iliyojengwa Kwa Kiwango Cha Lami Wilaya ya Magharibi "B" Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akipiga makofi baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Fuoni hadi Kombeni Wilaya ya Magharibi "B" Unguja na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi na 9kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Mhe.Dk. Sira Ubwa Mamboya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, wakipiga makofi baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la barabara wakiwa katika eneo la mwanzo ya barabara hiyo Kombeni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiondoa kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Barabara ya Kombeni hadi Fuoni iliojengwa kwa kiwango cha lami na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya. hafla hiyo imefanyika katika eneo la Kombeni Wilaya ya Magharibi "B".
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepe kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Kombe hadi Fuoni Wilaya ya Magharibi "B" Unguja iliyojengwa kwa kiwango cha lami na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar MheDk. Sira Ubwa Mamboya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akitembelea barabara mpya iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Kombeni hadi Fuoni Wilaya ya Magharibi "B" Unguja baada ya kuifungua leo 2/10/2020 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Mhe.Dk. Sira Ubwa Mamboya na (kushoto kwa Rais) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Mustafa Aboud Jumbe.
Baadhi ya Vijana wa Kijiji cha Kombeni Wilaya ya Magharibi "B"Unguja wakishuhudia ufunguzi wa barabara yao mpya inayowaunganisha na Fuoni wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Usafirishajin na Mawasiliano Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akitoa taarifa ya Kitaalam ya ujenzi wa Barabara ya Fuoni hadi Kombeni iliojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni kutoka Nchini China ya CCECC, wakati wa hafla ya ufunguzi wa barabara hiyo uliofanyika leo 2/10/2020. katika makutano ya barabara hiyo ya kombeni  na Fumba.
Waziri wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Mhe.Dk. Sira Ubwa Mambpoya akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa barabara ya Kombeni hadi Fuoni Wilaya ya Magharibi "B" Unguja, ufunguzi huo umefanyika katika eneo la Kijiji cha Kombeni leo Ijumaa.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa barabara ya Kombeni hadi Fuoni iliojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya Kichina ya CCECC,  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Kombeni na Fuoni wakati wa hafla ya ufunguzi wa barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya Kichina ya CCECC, ufunguzi huo umefanyika katika eneo la Kombeni Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo 2/10/2020.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa barabara ya Kombeni hadi Fuoni wakati mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani ) akiwahutubia katika eneo la Kombeni baada ya kuifungua barabara hiyo leo 2/10/2020.
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Wageni waalikwa wakifuatilia ufunguzi wa Barabara mpya iliyojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya Kichina ya CCECC. kutoka Kombeni hadi Fuoni.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.