Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan
Abbasi akizungumza na Watendaji wa Idara ya Utamaduni na Sera na Mipango wa
Wizara hiyo katika kikao cha kiutendaji kilichofanyika Novemba 24,Jijini
Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa wizara
hiyo Bw.Benard Marcelline.
Na Shamimu Nyaki –
WHUSM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan
Abbasi ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara hiyo kuanza
maandalizi ya kuzindua Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa.
Katibu Mkuu
Dkt.Abbasi ametoa maagizo hayo Novemba 24, Jijini Dodoma katika kikao chake na
Idara hiyo.
Dkt.Abbasi ameiagiza
Idara hiyo kusimamia vyema Taasisi zilizo chini yake hasa inayohusika na kukuza
na kuendeleza Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.
Aidha, Dkt. Abbasi ameitaka Idara hiyo kuratibu matamasha mbalimbali huku akieleza nia ya kuwa na tamasha la Singeli Festival mwishoni mwa mwezi Desemba, 2020.
No comments:
Post a Comment