Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Salim Hamad alipokuwa akiwasilisha Mada katika mafunzi elekezi kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Salim Hamad amesema matumizi mabaya ya
rasilimali za asili ikiwemo gesi na mafuta
ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kuwepo kwa migogoro ya kijamii.
Dkt. Salim amesema hayo wakati akiwasilisha mada
inayohusiana na maliasili na vyanzo vya migogoro ya kijamii katika mafunzo
elekezi kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani.
Amesema jamii
kadhaa ulimwenguni zinakabiliwa na migogoro mingi inayosababishwa na matumizi
mabaya ya rasilimali hizo, hivyo amewasisitiza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kusimamia
vyema Sekta hii kwa kutunga Sheria,Kanuni na miongozo bora na hatimae
rasilimali ya mafuta na gesi asilia kuweza
kuchimbwa kwa maslahi ya taifa zima.
Amewataka wajumbe hao kuangalia maeneo yote yanayoweza
kuleta changamoto na kuibua migogoro katika upatikanaji wa rasilimali ya mafuta
na gesi na kuyaainisha ili yaweze kupatiwa ufumbuzi mapema kabla ya utumiaji wa
rasilimali hizo.
Nao wa jumbe wa BLW kwa upande wao wameishukuru
taasisi ya ZPRA kwa kuandaa mafunzo hayo yatakayosaidia kutoa uelewa katika
muktadha wa kufahamu vyanzo halisi vya migogoro na namna bora ya kuitatua hasa
migogoro itokanayo na rasilimali za asili.
No comments:
Post a Comment