Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Amewataka Wananchi Kushirikiana Kuleta Maendeleo ya Jimbo

Takdir Suweid

Wilaya ya Magharibi B.  

Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Mhe.Ali Suleiman Mrembo amewataka Wananchi kushirikiana na Viongozi wao ili waweze kuwaletea maendeleo katika Jimbo lao.

Akizungumza katika ziara ya kuangalia kisima cha Gogobichi kilichopo kinuni amesema Ucahaguzi umekwisha kilichobakia ni Viongozi waliochaguliwa kurudi chini kusikiliza Wananchi kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Amesema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na baadhi ya Watu wasiojuilikana na kukiharibu kisima jambo ambalo limesababisha usumbufu wa upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wakaazi wa eneo hili na maeneo ya Jirani.

Aidha ameahidi kuwa Uongozi wa Jimbo la Pangawe utachukuwa hatua mbadala ikiwemo kupeleka Wataalamu wa kuangalia kisiama hicho na kuwapatia dawa ili waendelee kuyatumia maji ya kisiama hicho na kuwaondoshea usambufu wa kutafuta huduma ya maji safi na salama masafa ya mbali.

Hata hivyo amewaomba Wananchi amewaomba waendelee kudumisha Amani,Utulivu na kupendana ili mahusiano ya Wananchi yaendelee kuboreka na kuishi kwa salama na Amani.

Kwa upande wake Mwenyikiti wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Pangawe Dadi Juma Dadi wamelaani kitendo cha ufafuzi wa kisima hicho uliofanyika na kuliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kuwabaini waliofanya uchafuzi wa kisima hicho na kuhatarisha Afya za Wananchi wanaotumia kisiama hicho.  

Nao Wananchi wanaotumia kisiama hicho wameuomba Uongozi wa Jimbo kuwaangalia kwa Jicho la huruma kwani wanapata usumbufu mkubwa wa kufuata huduma hiyo masafa ya mbali na kutumia maji yasiokuwa safi na salama jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.