Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Dk Hussein Ali Mwinyi Atoa Salamu Katika Hafla ya Kuapishwa kwa Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Aupongeza utayari wa Rais Magufuli na kuahidi kumsaidia


RAIS wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali hassan Mwinyi ameupongeza utayari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  wa kuahidi kuwa mstari wa mbele kumsaidia katika kutekeleza yale yote aliyoyaahidi wakati wa Kampeni.

Rais Dk. Hussein Mwinyi aliasema hayo leo wakati akitoa salamu zake katika hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Mawaziri akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango, na Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profsa Kabudi hafla iliyofanyika leo huko Chamwino, nje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Mapema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli aliwaapisha viongozi hao na baadae baadhi ya viongozi walipata nafasi ya kutoa salamu zao akiwemo Rais Dk. Hussein Mwinyi.

 

Akitoa salamu zake hizo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alieleza imani kubwa aliyonayo Rais Magufuli kwake hatua ambayo inaonesha matarajio ya wananchi kwa kiongozi wao huyo pamoja na Serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema kuwa wananchi wa Zanzibar walikuwa na mategemeo makubwa kwa maisha yao bora baada ya uchaguzi mkuu.

Hivyo, matumaini hayo yamezidi kuimarika na kupanda mara baada ya kusikia hotuba ya Rais Magufuli katika ufunguzi wa Bunge la 12 wakati alipoahidi kuwa katika miaka mitano ijayo Seriali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoa ushirikiano mkubwa na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha, alisema kuwa wananchi hao wamezidi kupata matumaini kutokana na azma ya Rais Magufuli ya kuendelea kuisaidia na kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hivyo, Rais Dk. Hussein Mwinyi ameahidi kufanya kazi na kushirikiana na Rais Magufuli kwa azma ya kuleta maendeleo kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alimpongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Mawaziri wawili walioapishwa akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Hisdori Mpango pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

Rais Hussein Mwinyi alimpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majali Majaliwa kwa utendaji wake mzuri wa kazi hivyo kupata nafasi hiyo ni stahiki yake kwani aliwahi kwua bosi wake hivyo anautambua vyema utendaji wake.

Aidha, alimpongeza Waziri Mhe. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi na kueleza kwamba kwa vile suala la Mambo ya Nje ni la Muuungano hivyo, anaimanikuwa kuwa atafanya kazi nae kwa mashrikiano makubwa .

Rais Dk. Hussein Mwinyi alisema kuwa anaimani kubwa ya uongozi wa Waziri Philip Hisdori  Mpango katika masuala ya fedha hasa ikizingatiwa kwa Zanzibar na Tanzania Bara zinategemeana hivyo alimuahidi kushirikiana nae.

Rais Magufuli alimpongeza Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri wote walioapa huku akieleza kwamba hakuwa na haraka ya kuwachagua Mawaziri kwani bado mda upo hasa ikizingatiwa kwamba mara hii wako wengi.

Aliwataka Wabunge wasiwe na presha kwani kaziwaliyoomba ni Ubunge na sio Uawaziri hivyo waendelee kufanya kazinyaohiyo.

Hata hivyo, aliwataka viongozi hao kwenda  kuwatumikia wananchi kwani wananchi wameonesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara na Zanzibar hiyo imeoesha wazi kutokana na asilimia kubwa ya ushindi uliopatikana kwa Urais wa Zanzibar, Urais wa Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania pamoja na viongozi wote waliogombea  kwa tiketi ya CCM.

Nae Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alieleza imani aliyonayo Rais Magufuli kwa viongozi hao wote aliowateua inatokana na jinsi walivyomsaidia katika uongozi wake wa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Aliongeza kuwa katika uongozi wa Rais Magufuli hasa katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo aliwanyosha vizuri na kukubali kwamba walinyoka na kukiri  kuwa hivi sasa wamekuwa walimu wazuri na hivi sasa wanauwezo mkubwa wa kuwaongoza wenzao.

Mapema Rais Magufuli alimuapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Mawaziri wenzake hao wawili ambao walikula kiapo, walisaini kiapo pamoja na kula kiapo cha uadilifu kwa uongozi wa umma huku kila mmoja akitoa salamu zake.

Hafla hiyo ilitumbuizwa na Brasbandi ya Polisi pamoja na burudani za msanii maarufu Masanja Mkandamizaji.

 

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.