Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amemuapisha Katibu wa Rais Bw. Suleiman Ahmed Saleh Hafla hiyo Imefanyika Leo Ikulu 7/11/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Katibu wa Rais Bw. Suleiman Ahmed Saleh, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 7/11/2020.
 

RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi  amemuapisha Suleiman Ahmed Saleh kuwa Katibu wa Rais wa Zanzibar.

Hafla hiyo ya kiapo imefanyika leo Ikulu Jijiji Zanzibar.                                                                                                   

Rais Dk. Mwinyi amemuapisha Katibu huyo  baada ya  kumteua Novemba 4, mwaka huu kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Katika hafla hiyo viongozi mbali mbali walihudhuria, akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Hassan Khatib , Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Hassan Othman Ngwali, Viongozi wa Vikosi vya SMZ  pamoja na  viongozi mbali mbali kutoka Idara na taasisi mbali mbali za Serikali.

Kabla ya uteuzi huo Katibu huyo  alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya pamoja ya Fedha..

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 

 E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.