RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Bw.Sanjay Rughani alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazunguzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 18/11/2020 na kulia Mkuu wa Kitengo cha Masoko Bi. Juanita Mramba
Rais Dk.
Hussein Mwinyi alikutana na
uongozi wa Benki ya Standard Chartered ukiongozwa na Bwana Sanjay Rughani
ambapo katika maelezo yake Rais Dk. Hussein aliueleza uongozi huo kwamba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane imeahidi kufanya mambo mengi
kwa wananchi hasa kwa kushirikiana na Sekta binafsi.
Alisema kwamba Serikali iko
tayari kushirikiana na Taasisi mbali
mbali zimkiwemo za binafsi huku
akisisitiza kwamba miongoni mwa taasisi hizo sekta ya benki ni muhimu sana.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Nane imeahidi mambo mengi kwa
wananchi hivyo, mashirikiano na Benki ikiwemo Benki hiyo ya Kimataifa ya ‘Standard
Chartered’ ni muhimu katika kutekeleza miradi mbali mbali
ya maendeleo.
Alieleza kwamba iwapo ipo fursa ya kukaa pamoja na kujadili miradi ipi
ya kutekelezwa kwa pamoja Serikali iko tayari hasa ikizingatiwa kwamba Zanzibar
inahitaji wawekezaji kuja kuekeza katika maeneo mbali mbali.
Nae kiongozi huyo wa ujumbe huo
Sanjay Rughani alimpongeza Rais Dk. Hussein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa
Zanzibar na kueleza matarajio yake makubwa kutokana na ari na hamu ya Rais huyo
kuiletea maendeleo Zanzibar.
Kiongozi huyo alieleza kazi za Benki hiyo na namna inavyofanya kazi zake
ndani nan je ya Tanzania huku akieleza azma ya Benki hiyo ya kushirikiana na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sambamba na hayo, kiongozi huyo alieleza jinsi Benki hiyo inavyofanya
kazi na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na
Wizara ya Fedha ya Zanzibar pamoja na Benki mbali mbali hapa nchini ikiwemo
Benki Kuu (BOT).
Pamoja na hayo viongozi hao walieleza shughuli mbali mbali zinazofanywa
na Benki hiyo katika kuisaidia jamii ikiwemo kutoa huduma za tiba ya macho,
kuwasaidia watoto wa kike, uwekaji hakiba wa kifedha pamoja na mambo mengineyo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment