Habari za Punde

SERIKALI YAKEMEA WAZAZI WANAOSABABISHA UKATILI KWA WATOTO

Na Mwandishi Wetu Rukwa

Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendelo ya Jamii Dkt. John Jingu amekemea vitendo vya baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto kuandika majibu ya uongo ili wafeli mitihani na kuozeshwa, kuozwa  na watumikisha katika biashara.

Dkt. Jingu ameyasema hayo katika Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini Mkoani Rukwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto yaliyofanyika kwa ngazi ya mikoa.

Amewasisitiza  wazazi na walezi kutimiza wajibu wa kuwalea watoto kwa kuzingatia maadili na sio kujikita katika shughuli nyingine na hatmaye watoto kujiingiza katika matendo maovu.

 “Niseme wazazi na walezi tutumize wajibu wetu suala la malezi ya watoto ni letu sisi tusipotimkiza hilo tunatengeza jamii isiyo na maadili na uzalendo” alisema

Aidha Dkt. Jingu amewaasa watoto kutimiza wajibu wao kwa kuzingati masuala ya elimu na kuwaheshimu wazazi na walezi ili waweze kupata malezi bora na maadili mema kutoka kwao.

Awali akisoma risala kwa niaba ya watoto Lidya Ngogo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwezesha kupata elimu bora na kuwendelea kupambana na vitendo vya ukatili dhidi yao.

Kwa upande wake Omelina Mgawe kwa niaba ya wazazi amemuhakikishia Dkt. Jingu kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wanawafuatilia watoto wao katika masuala mbalimbali ikiweno elimu.

Nao baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Laela A wamshukuru Serikali kwa kutimiza haki ya kuendelezwa kwa watoto kwa kuhakikisha wanapoata fursa ya kuoata elimu kwa jinsi zote kwa usawa.

Wakati huo huo Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imetumia Siku ya Maadhimisho ya SIku ya Kimataifa ya Mtoto kuadhimisha miaka 30 ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki ya Mtoto wa mwaka 1989.

Tanzania imeungana na Nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto Kauli Mbiu isemayo: Dunia yenye Usawa kwa kila Mtoto inawezekana : Chukua Hatua

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.