Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji azungumza na watendaji wake asisitiza umoja na ushirikiano

 mfanyakazi masjala (ZIPA)  Pili Pongwa akitoa maelekezo kwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga kuhusu ucheleweshwaji wa vibali kwa wawekezaji, katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Chuo Cha Utalii Maruhubi Zanzibar.
Watendaji wa ZIPA wakimsikiliza Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga (hayumo pichani) wakati akitoa maelekezo juu ya utendaji wa Wizara hiyo huko Ukumbi wa chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar.
 Mfanyakazi masjala (ZIPA)  Pili Pongwa akitoa maelekezo kwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga kuhusu ucheleweshwaji wa vibali kwa wawekezaji,katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Chuo Cha Utalii Mruhubi Zanzibar.

Mfanyakazi masjala (ZIPA)  Pili Pongwa akitoa maelekezo kwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga kuhusu ucheleweshwaji wa vibali kwa wawekezaji,katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Chuo Cha Utalii Mruhubi Zanzibar.
 

PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO ZANZIBAR.


Na Sabiha Khamis      Maelezo      25/11/2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan Soraga amewataka wafanyakazi wa ZIPA kuwa na umoja na ushirikiano ili kufikia malengo na kuepuka ubaguzi, majungu na fitna ambazo zitazorotesha maendeleo ya ofisi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa ZIPA katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mkoa wa Mjini Maghari kufuatia agizo la Rais alilotowa mara baada ya kuwaapisha mawaziri.

 Amewataka wafanyakazi kuwa wazalendo kwa kuondoa ubaguzi wa aina yoyote kwa wawekezaji iwe kabila, dini, hata itikadi za vyama vyao ili kusimamia haki za watu kwa pamoja.

Aidha amewataka wafanyakazi kutowawekea vikwazo wawekezaji iwe wa nje au ndani ya Nchi kwa maslahi yao binafsi bali wawatumikie kwa maslahi ya nchi.

Pia amewashauri watendaji wa ZIPA kuwa wabunifu kwa kuweka njia mbadala ya kutafuta wawekezaji kwa kuitangaza Zanzibar mitandaoni na kupata wawekezaji  watakao kuingiza pato katika Serikali.

Vile vile ameahidi kutovumilia wala kufumbia macho uzembe, ubadhirifu na utoaji wa rushwa katika mazingira ya kazi ambayo yatapelekea kurudisha nyuma maendeleo ya Serikali na nchi.

“Sitovumilia uzembe, utoaji  upokeaji wa rushwa na ubadhirifu wa aina yeyote kwa watendaji wa serikali”alisema Waziri.

Aidha aliwataka kuweka utaratibu wa vikao vya mara kwa mara na wawekezaji ili kujua changamoto zinazowakabili ambazo zitapelekea kurudisha maendeleo ya uwekezaji huo.

Wakitoa changamoto zinazoikabili ZIPA baadhi ya wafanyakazi wamesema kwamba wanakabiliwa uhaba maeneo ya kufanyia kazi  na kuajiriwa kwa wafanyakazi wanaojitolea kwa muda mrefu.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.