Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais akutana na Uongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar {JUMAZA}

 Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar {JUMAZA} Sheikh Khamis Yussuf Khamis wa Tatu kutoka Kushoto akielezea majukumu yao wanayoyatekeleza katika maeneo mbali mbali wakati walipozungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman akizungmza na Ungozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akisisitiza umuhimu wa mashirikiano ya Viongozi na Jamii katika kupiga vita vitendo vha udhalilishaji  uliokthiri Nchini.

Picha na – OMPR – ZNZ.


Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Meshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema Jamii inaweza kuendelea kubakia salama endapo itajikubalisha kutafakari kwa kina jinsi itakavyoweza kuvitafutia dawa vitendo vya udhalilishaji Nchini vinavyoonekana kuwaathiri zaidi wanawake na Watoto wadogo.

Alisema Serikali tayari imeshajizatiti ikiwemo kufanya mabadiliko ya baadhi ya Sheria za kudhibiti vitendo hivyo viovu na kuitaka Jamii hasa Viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiraia kujumuisha nguvu zitakazokuwa muarubaini wa kuondokana na kadhia hiyo potovu.

Akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar {Jumaza} Ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman alisema inasikitisha kuona ongezeko la vitendo vya udalilishaji linatisha hasa ikitia huzuni Zaidi kuona wafanyaji wa uovu huo unahushisha pia Wazee wa Zaidi ya Umri wa Miaka Sabini.

Alisema nguvu za pamoja baina ya Viongozi na Wananchi hasa katika ngazi ya Shehia na Jimbo katika utoaji wa ushahidi dhidi ya Watu wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya Udhalilishaji hazitakuwa na kigugumizi kwa upande wa Polisi na Waendesha Mashataka.

Mheshimiwa Hemed Suleiman aliwataka Viongozi waendelee kuwahamasisha Wananchi kujenga tabia ya kutoa ushahidi pale wanaposhuhudia matukio ya vitendo vya udhalilishaji kinyume na hatua hiyo ni sawa na kusema kwamba hakuna hatua itakayoweza kuchukuliwa na wasimamizi wa sheria.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba Kiongozi ye yote atakayeshikwa kwa vitendo vya udhalilishaji Serikali itamuhesabu kama muhalifu na atalazimika kuchukuliwa hatua za kisheria bila ya kujali dhamana aliyokabidhiwa.

Mtendaji Mkuu huyo wa Shughuli za serikali alisisitiza umuhimu wa Jamii kubeba jukumu na dhima ya kuhakikisha Kizazi Kipya kinajikita katika kujitafutia Elimu zote mbili na kuacha mawazo ya uwepo wa masomo ya Sayansi pekee kitu ambacho ni upotovu.

Alisema wapo Wanafunzi wenye uwezo mkubwa wa ufahamu lakini baadhi yao tayari wameshajengwa vibaya na matokeo yake huathiri ukosefu wa Wataalamu kutokana na kundi kubwa kuelekea kwenye fani moja.

“ Miaka Kumi iliyopita tumeshuhudia hali ya kutisha iliyofikia wakati anatafutwa mwanafunzi wa fani ya sayansi anakosekana na kulazimika kutumia nguvu za ziada katika kuwaandaa ili kukidhi mahitaji halisi”. Alisema Mh. Hemed.

Akizungumzia changamoto ya ongezeko la mabaa katika mitaa mbali mbali Nchini, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Wazazi na Viongozi kutafakari na kufanya utafiti wa kubaini wanaoshiriki kwenye majengo hayo kama sio Watoto wao.

Alisema zipo changamoto zinazojitokeza kutokana na uwepo wa majengo hayo katika Jamii lakini asilimia kubwa ya wahusika wa vitendo vinavyoanzia kwenye majengo hayo vinatoka ndani ya Jamii inayowazunguuka Wazazi hao.

Mheshimiwa Hemed Suleiman aliwashauri Viongozi hao wa Jumuiya ya Muamsho Zanzibar kwa kushirikiana na Walimu wengine kutumia nafasi walizobarikiwa katika kufikisha Taaluma kwa umma jinsi ya kuepuka matendo maovu yanayochangia vurugu mitaani.

Aliwapongeza Viongozi hao kwa mchango wao wa kuendelea kuhimiza umuhimu wa uwepo wa Amani na Utulivu Nchini na kuwataka wazidi kuhubiri masuala hayo yatakayosaidia kuendelea kuiweka Nchi katika mazingira yatakayotoa fursa kwa Jamii kuendelea kutafuta riziki zao za kila siku.

Mapema Viongozi hao wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar { Jumaza} walisema katika kukabiliana na mporomoko wa Maadili katika Jamii wamelazimika kuanzisha Chuo cha mafunzo ya Ndoa kwa lengo la kurejesha hazina hiyo ya Maadili.

Walisema yapo matukio mengi ya ajabu miongoni mwa jamii hasa vijana yanayotishia hatma mbaya ya jamii jambo ambalo linaweza hata kuikosesha Serikali kupata nguvu kazi ya hapo baadae.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.