Habari za Punde

Mhe Hemed atoa siku tatu kuteketezwa mchele ulioharibika



AONYA SEREKALI HAITASITA KUMCHUKULIA HATUA MFANYABIASHA ATAKAEINGIZA BIDHAA MBOVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa  Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameonya vikali kwamba Serikali haitosita kumfutia kibali mara moja mfanyabiashara yeyote anayejihusisha na kuingiza bidhaa zisizokuwa na Kiwango Nchini.

Mhe. Hemed ametoa onyo hilo kali kufuatia ziara yake ya ghafla katika Bandari Kuu ya Malindi na kugundua uwezo wa Kontena Mbili zilizosheheni Mchele ulioingizwa Nchini na Mfanyabiashara Suleiman Abdulla tokea Mwezi Machi 2019 ambao tayari umeshaharibika.

Amesema anatoa siku tatu kuanzia leo kuhakikisha kwamba Makontena hayo yameshaondoshwa bandarini kwa kufuata taratibu za Kiafya na gharama za uondoshaji huo zitamsimamia Mfanyabiashara husika kama sheria inavyoelekeza.


Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Disemba 28, 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.