Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
alikutana na ujumbe kutoka nchini Oman na kubadilishana nao mawazo juu ya
maendeleo ya kulifanyia matengenzo makubwa jengo la Beit el Ajaib liliopo Forodhani
Jijini hapa pamoja na changamoto zilizojitokeza.
Dk. Mwinyi aliipongeza serikali ya Oman kwa juhudi kubwa inazozichukuwa katika kulifanyia matengenezo jengo hilo, kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano (MOU).
Amesema hatua ya kulifanyia matengenezo jengo hilo itasaidia kulirejeshea katika hali yake ya asili, na hivyo kuendelea kutumika na kuimarisha Utalii.
Aliishukuru Serikali ya Oman kwa msaada wake na hivyo kumuomba kiongozi wa ujumbe huo kumfikishia salamu za kheri kiongozi wa Taifa hilo.
Nae, Waziri wa Mambo ya Kale wa Oman Ibrahim Al Kharous alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kufuatilia kwa karibu matengenezo ya jengo hilo muhimu katika ustawi wa sekta ya utalii nchini.
Mapema, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.Mhe. Leila Mohamed Mussa alisema jengo la Beit al Ajaib ni muhimu sana katika maendeleo ya utalii nchini na kubainisha idadi kubwa ya wageni wanaolitembelea pale wanapozuru nchini.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024
2231822
E-mail: abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment