Habari za Punde

Vijana Waaswa kutotumia Dawa za kulevya

Na Takdir Suweid 

Wilaya ya Magharibi ‘’B’’                                                             21-12-2020.

 

Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Thuwaiba Jeni Pandu amewasisitiza Vijana kujiunga katika Vikundi vya Ujasiriamali ili kuweza kuelezea matatizo yao na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.


Amesema Serikali ya awamu ya 8 imetoa kutoa kipao mbele kwa Vijana lakini bila ya kujiunga pamoja itakuwa ni vigumu kuweza kuwafikia maeneo waliopo.

 

Akizungumza na Vijana wa kikundi cha Safina Pangawe Bondeni katika Mkutano wa kujadili matatizo yanayowakabili amesema Serikali imeweka mikakati ya kuwasaidia Vijana katika maeneo yao ili waepukane na hali tegemezi.

 

Hivyo ameahidi kushirikiana na Viongozi wenzake, kuhakisha malengo ya kuwaenua Vijana kiuchumi, kisisa, kiutamaduni yanafanikiwa,maeneo ya Mjini na Vijjini.

 

Aidha amewataka Vijana hao kufanya kazi kwa bidii na kuacha kujishirikisha na Vitendo vya Utumiaji wa Dawa za kulevya ili wabaki kuwa Vijana imara na wenye nguvu za kuijenga nchi yao.

 

Kwa upande wake Hassan Ali Muhammed ambae ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho amesema tokea kuanzishwa kwa kikundi chicho mika 10 ilipita, hawaajapata msukumo wowote licha ya kuomba Msaada sehemu mblimbali. hivyo wamewaomba Viongozi wa Jimbo kuwaunga Mkono ili waeweze kufikia malengo waliojipangia.

 

Nao baadhi ya Vijana hao wameomba kupatiwa ufumbuzi tatizo Ukosefu wa Ajira, Mitaji ya kuanzisha Vikundi, Vifaa vya Michezo na Sanaa ili waweze kujijiri na kuuipunguzia mzigo Serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.