Habari za Punde

Serikali kusimamia vyema maslahi yake kwenye kuungana na Kampuni za Simu za Mkononi ya Zantel na Tigo kwa ajili ya maslahi ya Umma.


 Waziri wa Nchi, Afisi Ya Rais Ya Fedha na Mipango Zanzibar  Mheshimiwa Jamal Kassim Ali amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itasimamia vyema maslahi yake katika Kuungana kwa Kampuni za Simu za Mkononi ya Zantel na Tigo kwa ajili ya maslahi ya Umma.

Aidha Mheshimiwa Jamal amesema mahitaji ya Serikali ni kuona ubia wa Serikali unakuwepo kama awali kwa upande wa Zantel ikiwa ni pamoja na kushiriki katika masuala ya maamuzi na Serikali kupata kodi yake na kuimarika kwa huduma za mawasiliano.
Mheshimiwa Jamal amesema Serikali ya awamu ya nane imejikita zaidi katika kuitumikia jamii ili iweze kuleta maendeleo ya haraka na kukuza uchumi wa Nchi yetu.
Waziri Jamal amesema kuwa Mapinduzi ya kiuchumi yanayotokana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hivyo Serikali itajikita kuona inaitumia fursa hiyo. Amesema Mifumo ya kutumia miamala ya kusafirisha Fedha kupitia Simu za Mkononi imesaidia kutanuka kwa Biashara na kubadilisha maisha ya Wananchi Kiuchumi na Kijamii.
Mheshimiwa Jamal ameyasema hayo hapo jana Ofisini kwake Vuga alipozungumza na Viongozi wa Kampuni hizo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Melcon iliosimamia Muungano wa Kampuni ya Zantel na Tigo Balozi Amir Mpungwe ameipongeza Serikali kwa kuwaunga Mkono katika kufanikisha hatua waliofikia.
Hata hivyo amesema Sekta ya Mawasiliano imesaidia katika kuwawezesha Wananchi kufanya miamala ya Fedha, kutoa Ajira na kulipa kodi ya Serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.