Habari za Punde

Dk Mwinyi awapongeza Madaktari Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Daktari Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dkt. Said Idrisa Ahmada, walipofika ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kupongezwa kwa kufanikisha uporeshaji ya Raia wa Nigeria Bi.Kelesh Belinda, iliofanywa na Kitengo cha Upasuaji Hospitali ya Kuu ya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati Profesa Jose Piquer Belloch Rais wa Taasisi ya NED ya Nchini Hispania, wakati  mazungumzo na kupongezwa kwa Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hopitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwapongeza Madaktari Bingwa Wazalendo wa Hospital ya Mnazi Mmoja wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (hawapo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
MADAKTARI Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya kupongezwa kwa kufanikisha upasuaji wa Raia wa Nigeria Bi. Kelesh Belinda, uliofanywa katika Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu ikiongozwa na Dkt. Said Idrisa Ahmada.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Kitengo cha Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar baada ya kumaliza mazungumzo yake na kuwapongeza kwa kazi nzuri, na waliokaa (kulia kwa Rais) Rais wa Taasisi ya NED ya Nchini Hispania Prof.Jose Piquer Belloch, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Zanzibar Dkt.Omar Dadi Shajak na Daktari Bingwa wa Upasuaji Ubongo Mishipa ya Fahamu Dkt.Said Idrisa Ahmada na( kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said Dkt.Abdalla Hasnu Makame na Dkt Juma Mambi.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.