Habari za Punde

Mabalozi wa CCM watakiwa kuwasaidia viongozi waliowachagua

 Mwashungi Tahir  Maelezo          14-2-2021.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Kichama Talib Ali Talib amewataka Mabalozi kuwasaidia Viongozi wao waliowachaguwa na kuacha kuwasema vibaya Mitaani.


Amesema Chama Cha Mapinduzi kimeweka utaratibu mzuri wa kukosoana hivyo ni vyema kutumia vikao kwa kupeleka malalamiko yao katika sehemu husika ili yaweze kufanyiwa kazi.


Akizungumza na Mabalozi wa Jimbo la Magomeni katika Ukumbi wa  Magae uliopo Meya wakati alipokuwa akikabidhi fedha taslim sh.miloni 10 zilizotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo ikiwa ni ahadi alizoziweka kwa mabalozi hao wakati wa kampeni za Uchaguzi.


Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi katika Mkoa huo hakiko tayari kusikia Viongozi wanasemwa vibaya na badala yake waungwe mkono ili watekeleze majukumu yao na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya nane katika kuondosha Ubadhirifu, Uvivu na Uzembe.


Hata hivyo amewasisitiza Vingozi wa Mjimbo kushuka chini kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025.


Nae Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni  Jamal Kassim Ali amesema ameamua kukabidhi sh. Milioni 10 kwa Mabalozi hao kwani ndio dira ya Maendeleo katika kushughulikia na kuimarisha Chama hivyo Viongozi wataendelea kuwathamini na kuwajali kutokana na utendaji wa kazi zao.


Mh.Jamal ambae pia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ameahidi kuboresha maslahi ya Watendaji kadri hali inavyoruhusu ili kuongeza Ari na Ufanisi wa Kazi zao wanazozifanya katika jimbo lao .


“Kwa vile mumeniamini na kunipa kura nyingi na mimi sinabudi kurudi na kutoa shukurani kama Rais wetu anavyohimiza kwa kutimizaahadi zangu ambazo niliahidikatika kipindi hicho”, alisema Mwakilishihuyo.


Nao Mabalozi hao wamewaomba Viongozi kuwa karibu nao ili kuweza kujuwa Matatizo yanayowakabili ndani ya Jimbo hilo na kukaa nao pamoja kwa  kuayapatia Ufumbuzi wa haraka kadiri iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.