Habari za Punde

Mhe Hemed mgeni rasmi katika ufunguzi wa Tamasha la Choma Choma katika Viwanja vya Fumba City Park

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akishiriki Tamasha la Choma Choma, lililokwenda sambamba na kuchangia kumaliza kwa ujenzi wa Nyumba ya Watoto Yatima wanaoishi na virusi vya Ukimwi lilofanyika Viwanja vya Fumba City Park.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Zanzibar Aids Association and Support of Orphans (ZASO childrens Home) Abdu Bwana Maulid Haji akitoa Taarifa ya Kituo cha Taasisi hiyo
Mlezi wa Taasisi ya Zanzibar Aids Association and Support of Orphans (ZASO childrens Home) Mh. Mgeni Hassan Juma akielezea malengo ya baadae ya Kituo cha Taasisi hiyo
Spika wa Baraza ;a Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulid akitoa salamu maalum kwenye Tamasha la Choma Choma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na washiriki wa Tamasha hilo la Choma Choma hapo Viwanja vya Fumba City Park.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akiwa payika picha ya pamoja na Viongozi walioshiriki Tamasha la choma choma lililofanyika katika Viwanja vya Fumba City Park.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, ameitaka jamii kuishi vyema na watoto Yatima, kwa kuwapa fursa zote stahiki, na kuwasihi wale wanaowanyanyapaa kuacha tabia hiyo, mara moja, ili watoto hao waendelee kuwa na furaha ya moyo kama walivyo watoto wenzao.

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, ameyasema hayo katika sherehe ya ufunguzi wa Tamasha la Choma Choma katika Viwanja vya Fumba City Park, iliyoandaliwa na kampuni ya Dafu kwa kushirikiana na Taasisi ya Zanzibar Aids Association and Support of Orphans (ZASO childrens Home).

Ameeleza kwamba kuwasaidia watoto Yatima mbali ya kupata fungu mbele ya Mwezi Mungu, lakini pia ni kujisaidia wenyewe kwani bila ya kufanya hivyo baadae Jamii inaweza kupata   wototo watakaojiingiza katika vitendo viovu na vya kihalifu .

Mheshimiwa Hemed alisema Zanzibar ina mahitaji mengi ambayo serikali pekee haiwezi kuyasimamia na kuyakamilisha , hivyo ni vyema jamii na watu wenye uwezo kuendelea kusaidiana na serikali,akitolea mfano wa kituo cha ZASO, na kusema kuwa ni mfano wa kuigwa hapa Nchini.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid amesema kutokana na mahitaji maalum ya watoto hao kuna haja kwa serikali kukiangalia kituo hicho kwa jicho la karibu ili kuwapatia mahitaji ya msingi watoto hao.

Mhe. Zubeir amemesa ni vyema serikali kubuni mipango ya kudumu itakayowasaida watoto hao katika kuwahudumia moja kwa moja, kwa lengo la kukipunguzia mzigo kituo hicho, sambamba na kuwaomba  wadau wengine kuwa tayari kutoa mashirikiano yao muda wowote itakapohitajika.

Nae Mlezi wa kituo hicho, ambae pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilisihi Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma alisema lengo la kuwepo kwa kituo hicho, ni kuwasaidia watoto yatima wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi, ili kupata haki stahiki kama walivyo watoto wengine, bila ya kujali hali waliyo  nayo, ikiwemo kuishi, kusoma na haki nyengine.

Sherehe za Ufunguzi wa Tamasha la Choma Choma, limeenda sambamba na kuchangia kumaliza kwa ujenzi wa Nyumba ya Watoto Yatima wanaoishi na virusi vya Ukimwi, pia imepambwa na burudani  kutoka kwa wasanii mbali mbali nchini.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.