Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amefanya Uteuzi Kamishna wa ZRB na Mkurugenzi Mwendeshaji PBZ

 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  amefanya uteuzi mpya wa Kamishna wa Bodi ya Mapato (ZRB), pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Kwa upande wa Bodi ya Mapato (ZRB), alieteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi hiyo ni Salum Yussuf Ali, uteuzi ambao umeanza tarehe 10 Februari,2021.

Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi amemteua Muhsin Salim Masoud kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kuanzia tarehe 10 Februari, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, Kamishna wa Bodi ya Mapato (ZRB) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) waliotenguliwa watapangiwa kazi nyengine kadri itakavyoamuliwa.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.