Habari za Punde

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Aongoza Wakuu wa Idara na Vitengo Kupitishwa Mfumo wa Ofisi Mtandao Jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akijadiliana na Afisa Kumbukumbu, Hashim Salum (kulia) na Afisa Tehama wa wizara hiyo,Robert Mberesero (katikati), wakati wa mafunzo ya kuwapitisha Wakuu wa Idara na Vitengo katika Mfumo wa Ofisi Mtandao utakaonza kutumika serikalini ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma.Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Makao Makuu ya wizara jijini Dodoma
Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Felix Changwe(kulia) na Afisa TEHAMA wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Robert Mberesero(kushoto),wakiwapitisha katika Mfumo wa Ofisi Mtandao wakuu wa vitengo wa wizara hiyo(waliokaa),wakati wa mafunzo ya mfumo huo wenye lengo la kuboresha utolewaji huduma. Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Makao Makuu ya wizara jijini Dodoma
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Abas Malekela (kushoto) na Msajili wa Taasisi za Kijami na Kidini, Emmanuel Kihampa wakiupitia  Mfumo wa Ofisi Mtandao wakati wa mafunzo hayo  ambao lengo la mfumo huo ni kuboresha utolewaji wa huduma serikalini. Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Makao Makuu ya wizara jijini Dodoma
Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Felix Changwe (aliyesimama),akimpitisha Mkurugenzi wa Kitengo cha Malalamiko wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kamishna Albert Nyamhanga katika Mfumo wa Ofisi Mtandao ambao una lengo la kuboresha utolewaji wa huduma serikalini.Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Makao Makuu ya wizara jijini Dodoma.

Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.