Habari za Punde

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Wizara ya Fedha na Mipango wakipeleka miti katika eneo la upandaji katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma kuelekea sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Gisela Mugumira (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Agatha Madalle (kulia) wakijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe wa TUGHE wakati wa zoezi la upandaji miti katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya kutunza mazingira ikiwa ni maandalizi ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.

Wajumbe wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha zoezi la kupanda miti katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.