Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefika Hospital ya Mnani Mmoja Kuwafariji Majeruhi Waandishi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimfariji na kumpa pole Mpiga Picha wa Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Hassan Issa, aliyelezwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, baada ya kupata ajali wakiwa katika msafara wakielekea Mkoa wa Kusini Unguja leo asubuhi. 

Rais Dk. Mwinyi alifika Hospitali kuu ya Rufaa ya MnaziMmoja kwa ajili ya kuwakagua majeruhi wa ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo huko Kitogani, Mkoa wa Kusini Unguja ambayo imewahusisha wafanyakazi wa kitengo cha habari cha Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Akiwa ameongozana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Rais Dk. Mwinyi alipata fursa ya kuwakagua majeruhi hao waliopata ajali hiyo na kuwaombea kupona kwa haraka huku akimuombea kwa Mwenyezi Mungu kumlaza mahala pema peponi mmoja wa wafanyakazi hao aliyefariki dunia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.