Habari za Punde

Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Kwenye Miradi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na Makazi ya Askari Oljoro Jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anold Kihaule (kulia), akitoa maelezo leo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama waliofika katika Mradi wa Uunganishaji Mtandao wa Mawasiliano kati ya Vituo vya Usajili na Makao Makuu uliopo jijini Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama wakimsikiliza Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) walivyofika katika Mradi wa Uunganishaji Mtandao wa Mawasiliano kati ya Vituo vya Usajili na Makao Makuu uliopo jijini Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mussa Azan Zungu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha,leo  wakati akiwasili kwa ajili ya kuwaongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama kukagua nyumba mpya za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika Kambi ya FFU jijini Arusha
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama,Mussa Azan Zungu(katikati),akiwa ndani ya nyumba mpya za askari polisi zilizojengwa katika Kambi ya FFU iliyopo Oljoro jijini Arusha leo, ikiwa ni mkakati wa serikali kutatua changamoto ya makazi ya askari nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.