Habari za Punde

Kamanda Mtafungwa Atoa Onyo Kwa Madereva Walevi Nchini.

KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilboard Mtafungwa amewataka ametoa onyo kali kwa madereva wa malori na mafuso hapa nchini ambao wamekuwa wakiendesha magari nyakati za usiku wakiwa wamelewa waache tabia hiyo mara la sivyo watajikuta wakiishia kwenye mikono ya sheria.

Mtafungwa aliyasema hayo akiwa mkoani Tanga wakati alipokuwa akiongea na madereva ,sambamba na watoa huduma wa mabasi juu ya masuala ya usalama barabarani  kwenye kituo cha Stendi ya Mabasi Kange na eneo la Mabanda ya Papa alipozungumza na madereva wa malori.


Alisema kwamba wapo baadhi ya madereva ambao wamekuwa wakiendesha magari hayo wakitokea Dar es Salaam wanasubiri mpaka gizo liingie kwa kisingizio kwamba serikali,Jeshi la Polisi itakuwa imelala wanakaa sehemu wanaanza kunywa pombe matokeo yake wanakwenda kuendesha magari wakiwa wamelewa.


“Madereva mnaoendesha Malori ,Mafuso wakiwa wamelewa ndugu zangu niwaambie kwamba maisha yenu yana thamani kubwa sana na kuishi ni mara moja hakuna kuishi mara mbili lazima mjali maisha yenu wewe umetoka na fuso Dare s Salaam unasuburi  mpaka giza liingie kwa kisingizio kwamba serikali itakuwa imelala polisi sasa wewe ulali unakaa sehemu unaanza kunywa na pombe matokeo yake unakuja kuendesha gari ukiwa umelewa”Alisema


Alisema kwa  sasa hayo wamekwisha kuyabaini na wameweka utaratibu wa kuwakagua hata nyakati za usiku RTO pelekeni askari wakiwa wamevaa kiraia au sare  wahakikisheni wanawakagua mpaka usiku lori ambalo linatiliwa walisimamishe wapime ulevi madereva kwa sababu wanavyo vya kutosha wakigundua wamekunywa pombe wamelewa wamakatwe wakae ndani mpaka pombe zake ziishe na baadae wawapeleke mahakamani.


Kamanda Mtafungwa alisema hatua hizo ni kubwa na hawataki zichukuliwe wanataka kila mtu athamni kazi anayofanya lakini niwaambie wale walevi kaeni chonjo hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yenu kutokana na kutokufuata sheria zilizopo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.