Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji Wake Rais wa Uganda Mhe Museveni Washuhudia Utiaji wa Saini Mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki Ikulu Entebe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebe mchache kabla viongozi hao kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha ratiba ya hafla  ya uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga baada ya yeye na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kuombwa na Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya Total duniani Bw. Patrick Poyanne kufanya hivyo ili iwe kumbukumbu yake ya
siku hiyo ya kihistoria katika Ikulu ya Entebbe leo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Dkt James Mataragio akiweka saini kwa niaba ya Tanzania mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga katika hafla iliyofanyika leo Ikulu ya Entebbe na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.