MAKAMU wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, akifungua msikiti wa Masjid
Riyadhi-Swaalihina Uliopo Mgogoni Wilaya ya Chake Chake, kwa niaba ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dk.Hussein Ali Mwinyi.
MAKAMU wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla (katikati), Mufti Mkuu wa Zanzibar
Alhaj Shekh Saleh Omar Kabi, wakiwaongoza Viongozi mbali mbali wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wa Mgogoni katika sala ya Ijumaa,
iliyosalishwa na Ustadhi Muhyiddin Makame Hamad, mara baada ya kuufungua masjid
Riyadhu-Swaalihina Mgogoni
MWALIM Ali Juma
Khamis akisoma risala ya wanakijiji cha Mgogoni Wilaya ya Chake Chake, kwa
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, baada ya kuufungua
Rasmi Masjid Riyadhu-Swaalihina kwa niaba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaji Dkt.Hussein Ali Mwinyi
MUFTI Mkuu wa
Zanzibar Alhaj Shekh Saleh Omar Kabi, akitoa salamu zake kwa waumini wa dini ya
Kiislamu kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, huko katika Masjid
Riyadhu-Swaalihina Mgogoni Wilaya ya Chake Chake
MAKAMU wa Pili wa
Rias wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, akitoa salamu za Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi, kwa wananchi wa
Mgogoni, mara baada ya kuufungua Rasmi Masjid Riyadhu-Swaalihina Mgogoni Wawi
Chake Chake Pemba.
VIONGOZI mbali mbali wa Serikali na wananchi wa kijiji cha Mgogoni Wilaya ya Chake Chake, wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Masjid Riyadhu-Swaalihina Mgogoni.
(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment