Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.
Faustine Ndugulile akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti Bungeni, Dodoma. Aliyeketi
wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na wa kwanza
kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Anne Kilango Malecela
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu, Seleman Kakoso akizungumza baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi mbele katikati) kuwasilisha
taarifa kuhusu mawasiliano na intaneti kwa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma. Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, akimsikiliza.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu, Anne Kilango Malecela akichangia mada baada ya Waziri wa Mawasiliano
na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha
taarifa kwa Kamati hiyo kuhusu mawasiliano na intaneti Bungeni, Dodoma.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akichangia hoja kwenye
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu baada ya Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha
taarifa kuhusu mawasiliano na intaneti kwa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dkt. Jabir Bakari akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu baada ya Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa kuhusu mawasiliano na intaneti kwa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma. Wa kwanza kulia ni Katibu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na katikati ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi.
No comments:
Post a Comment