Habari za Punde

Sirro amvalisha cheo Kamishna Hamduni

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kulia) akimvalisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Hamdun kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya Mhe. Rais kumpandisha cheo kuwa kamishna wa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ndogo ya Polisi jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimkabidhi Kamishna wa Polisi CP Salum Hamdun, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kitabu cha Muongozo kinacholiongoza Jeshi la Polisi baada ya kumvalisha Cheo cha Ukamishna kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya Mhe. Rais kumpandisha Cheo kuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo imefanyika leo Makao Makuu ndogo ya Polisi jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.