Habari za Punde

Wananchi Watakiwa Kuchukua Tahadhari Ushauri Kwa Umma.

 

USHAURI KWA UMMA

Katika kuadhimisha Sikukuu ya Eid el Fitr, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, inachukua nafasi hii kutoa ushauri kwa wananchi juu ya kuchukua tahadhari wakati wa mikusanyiko ili kuepuka maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa kujiweka mbali na mazingira yanayoweza kupelekea kufanya au kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji au kufanya ngono na mtu asiye stahiki.

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, inasisitiza kuchukua tahadhari kwa kufanya yafuatayo:

1.    Epuka ngono, Usimuamini mtu. Huenda akawa ameambukizwa VVU

2.    Epuka michanganyiko ya faragha au sehemu zenye giza

3.    Jiepushe na unywaji wa pombe na utumiaji wa dawa za kulevya unaweza kusababisha kuambukizwa VVU kwa kufanya ngono zembe.

4.    Vaa kivazi cha stara kuepuka kuvunjiwa heshima.

5.    Epuka matembezi wakati wa usiku mkubwa

6.    Toa taarifa kwa vitendo vyovyote vya udhalilishaji kwa mzazi na katika vyombo vya usalama

Tukiweza kuyafanya haya, tutasheherekea sikukuu ya Eid el fitr kwa salama bila ya maambukizo ya Virusi vya UKIMWI.

Kulu A’amin wa Antum Bikhayr  EID MUBARAK kwa wananchi wote.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS.

ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.