Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Amejumuka na Wananchi na Familia Katika Maziko ya Wahanga wa Ajali ya Basi Mkoani Shinyanga.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akishiriki sala ya maiti kufuatia kifo cha Marehemu Wahda Yussuf aliesaliwa katika Masjid Fatma Kwahani. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiweka mchanga kaburini wakati waumini wakiustiri mwili wa marehemu Wahda Yussuf katika makaburi ya Mwanakwerekwe
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Idrisa Kitwana Mustafa akiweka mchanga kaburini wakati waumini wakiustiri mwili wa marehemu Wahda Yussuf katika makaburi ya Mwanakwerekwe.

  Picha na OMPR

Na Kassim Abdi, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewaongoza waaumini katika kuusitiri mwili wa Marehemu Wahda Yussuf aliefariki kufuatia ajali ya basi iliotokea Mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia Jana iliyojumuisha wanafunzi wengine kutoka Zanzibar.

Mhe. Hemed akiambatana na viongozi wa serikali pamoja na watendaji wa serikali walishiriki katika sala ya maiti iliosaliwa katika Masjid Fatma Kwahani.

Harakati za kuustiri mwili wa marehemu zimefanyika katika makaburi ya waislamu ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Makamu wa Pili wa Rais alishiriki katika harakati hizo za mazishi ikiwa ni  utekelezaji wa ahadi ya serikali katika kusimamia na kugharamia taratibu zote za msiba.

Mapema jana usiku, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla,  alizifariji Familia za marehemu hao waliofika katika Kiwanja chya ndege cha kimataifa cha Abeid Amani Karume  kwa kusema

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed alizitaka familia hizo kuwa na subira kutokana na msiba huo uliotokea ambao umegusa nyoyo za wananchi wote wa Zanzibar.

Maiti zilizowasili Zanzibar kutokea mkoani Shinyanga ni Rehema Haji Juma aliezikwa Kijijini kwao Kizimukazi

Wahda Yussuf aliezikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe na Nassor Juma Khamis aliezikwa Bububu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.