Habari za Punde

Uturuki na SMZ Kushirikiana Kutoa Elimu ya Mafunzo ya Amali Pamoja na Kujenga Chuo Cha Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed said (katikati) pamoja na Waziri wa Fedha mhe, Jamal Kassim Ali wa kwanza kulia, wakiwa katika ofisi ya Jumuiya ya Turkish Maarif  wakifanya  mazungumzo na Naibu Waziri wa Elimu wa Uturuki Mr. Mahmut Ozer, kwa lengo la kuimarisha na kujenga chuo cha Amali Zanzibar.
Naibu Waziri wa Elimu wa Uturuki Mr. Mahmut Ozer, akimkabidhi zawadi ya Nembo maalum, Waziri wa Fedha Mhe ,Jamal Kassim Ali baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Na.Maulid Yussuf WEMA.

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiangalia wanafunzi wa darasa la maandalizi namna wanavyofundishwa masomo ya mafunzo ya Amali  Katika Skuli ya Serikali na binafsi nchini Uturuki.

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mhe Simai Mohammed Said ambae ni Waziri wa.Elimu na Mafunzo ya  Amali akiwa pamoja na Waziri wa Fedha Mhe Jamal Kassim Ali, wakiwa Katika ziara yao nchini Uturuki katika Skuli ya binafsi ya YENIDOUGUOKULLARI A.S BASAKSEHIR KAMPUSU wakiangalia namna wanafunzi wanavoanza kufundishwa elimu ya Amali kuanzia maandalizi katika Skuli hiyo.

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika ziara yao nchini Uturuki pamoja na wenyeji wao, kufuatia muwaliko maalum waliopewa na Jumuiya ya Turkish Maarif ya nchi Hiyo.

Picha na Maulid Yussuf WEMA.

Na Maulid Yussuf  - WEMA Uturuki.                                                                                                                   

Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wameanza ziara yao leo nchini Uturuki kufuatia muwaliko maalum waliopewa na Jumuiya ya Turkish Maarif ya nchi hiyo kwa lengo la kujifunza pamoja na kuangalia uwezekano wa kuimarisha Mafunzo ya Amali ya Zanzibar. 

Wakiwa katika ziara yao hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe, Jamal Kassim Ali wamefika katika ofisi ya Jumuiya ya Turkish Maarif na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Elimu wa Uturuki Mr. Mahmut Ozer, ambae amekubali  kushirikiana katika kutoa elimu ya Mafunzo ya Amali pamoja na kujenga Chuo cha Mafunzo ya Amali Zanzibar ili kurahisisha utoaji wa huduma hiyo Zanzjbar.  

Mawaziri hao wamemshukuru Naibu waziri huyo kwa kuwakubalia maombi yao ambapo wameahidi kuendeleza mashirikiano yao ili kuleta maendeleo katika nchi hizo.

Pia katika ziara yao Mawaziri hao walitembelea Skuli binafsi ya Yenidoguokullari A.S Basaksehir Kampusa, pamoja na Skuli ya Serikali ya Uturuki Kanikoy Ahmet Sani Gezici Kiz  Anadolu İmam Hatip Lisesi,, ambazo zote zinafundisha masomo mbali mbali ikiwemo somo la Elimu ya Amali na kuona namna somo hilo linavyoanza kufundishwa tokea darasa la maandalizi. 

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Serikali ya Uturuki KANIKÖY AHMET SANİ GEZİCİ KIZ ANADOLU İMAM HATİP LİSESİ, PROF. AYSEN GŰRCAN, amesema amefarajika kufikiwa na.ugeni kutoka Zanzibar ambapo amesema ana imani wataweza kujifunza mengi kutoka nchi yao huku akiwaomba kuendeleza ushirikiano huo katika masuala mbalimbali pamoja na.kumuomba mhe Simai kufanya ziara za.kimasomo kati ya nchi skuli yake na Skuli za Zanzibar.

Ziara ya Mawaziri hao inaendelea kwa kuonana na kuzungumza na Shirikisho la Wafanya biashara la Instanbull pamoja na kuonana na Mwenyekiti wa chama Tawala cha  AK PARTI cha Instanbul,  mr OSMAN NURI  pamoja na Kutembelea chuo cha Ufundi cha Uturuki  kinachoitwa HAYDARPASA TECHNICAL COLLEGE.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.