Habari za Punde

HESLB YAMPONGEZA RAIS SAMIA ONGEZEKO LA BAJETI MIKOPO ELIMU YA JUU

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga  (kushoto)akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru wakati alipotembelea Banda la HESLB leo Jumamosi Julai 31, 2021 wakati wa kufunga  Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika kuanzia tarehe 26-31 Julai, 2o21 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga wa (pili kushoto) akizungumza na Mbunge wa Zamani Mkoa wa Pwani, Dkt. Zainab Gama (kulia) wakati alipotembelea Banda la HESLB katika Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yalianza tareh2 26-31 Julai mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru.

  Afisa Mikopo Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Juu (HESLB), Mchunga Simba akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa vyombo vya habari leo Jumamosi Julai 31, 2021 wakati wa kufunga maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyohimishwa leo Jumamosi Julai 312, 2021 katika Viwanja vya MnaziMmoja Jijini Dar es Salaam.  

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 31.7.2021

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua ya Serikali kuongeza bajeti ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2021/2022 yenye kiasi cha TZS 570 Bilioni iliyoweka historia katika taasisi hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi tarehe 31 Julai, mwaka huu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema ongezeko la bajeti hiyo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya kusaidia Watanzania wahitaji.

Badru alisema katika bajeti hiyo yenye uwezo wa kusomesha wanafunzi 160,000, imewalenga wanafunzi wahitaji wanaotokea katika kaya zisizojiweza na hivyo kuwataka kuhakikisha kuwa wanakamilisha taratibu za maombi kama zilivyoanishwa katika mwongozo wa uombaji mikopo wa mwaka 2021/2022.

Kwa mwaka jana bajeti yetu ilisomesha wanafunzi 55,000 wa mwaka wa kwanza na kwa mwaka huu tunaratajia kusomesha wanafunzi 62,000 hii ni idadi kubwa kwa mwaka huu, tunawaomba wanafunzi wahitaji kuhakikisha wanaomba kwa usahihi” alisema Badru.

Akizungumzia kuhusu hali ya urejeshaji Mikopo, Badru alisema kwa sasa kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanafunzi wanufaika kurejesha mikopo yao kwa hiari, hatua iliyotokana na Serikali kufuta tozo na adhabu mbalimbali zilizokuwepo awali.

Kuanzia Mwezi Julai mwaka huu, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanufaika kurejesha mikopo yao, na hapa katika maonesho tumeshuhudia wanufaika wengi wakifika katika Banda kwa ajili ya kupata taarifa za madeni ya mikopo” alisema Badru.

Aidha Badru alisema HESLB itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo waajiri ili kuhakikisha kuwa madeni ya mikopo kutoka kwa wanafunzi wanufaika inarejesha ili kuiwezesha Serikali kuwa na Mfuko endelevu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.