Habari za Punde

PSSSF YAENDESHA SEMINA KWA WASTAAFU DODOMA

MTAKA: Semina za kustaafu zianze kwa Vijana

*Ashauri Watumishi kujipanga vyema kustaafu

*Aipongeza PSSSF kwa kuandaa semina

*PSSSF: Semina hizi ni endelevu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Anthony ameushauri Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwashirikisha Vijana wanaoanza kazi katika mafunzo ya kujiandaa kustaafu kwani mipango ya kustaafu huanza pale mtu anapoajiriwa.

Bw. Mtaka alitoa ushauri huo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua semina kwa Wastaafu wataraji wa PSSSF kwa wananchama wa Mfuko huo mkoani Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Bw. Anthony Mtaka akizungumza wakati akifungua semia kwa Wastaafu watarajiwa wa PSSSF wa jijini Dodoma.

“Maandalizi ya kustaafu yanaanzia pale mtu anapoajiriwa, hivyo ni vyema katika semina zijazo mkawashirikisha vijana ili waweze kujipanga vyema kwa ajili ya maisha yao baada ya ajira” alishauri Bw. Mtaka.

Mkuu huyo wa mkoa aliwashauri wastaafu kufanya miradi watakayoimudu baada ya kustaafu na kuachana na miradi ambayo itawaigiza katika matatizo.

“Hakikisha unachagua mapema sehemu ambayo utaishi baada ya kustaafu, andaa vyema kitu utakachofanya, achaneni na miradi itakayowafanya mkope na kubwa kuweni makini na matumizi yenu”alishauri Bw.Mtaka.

Bw. Mtaka aliipongeza PSSSF kwa kuandaa mafunzo kwa Wastaafu watarajiwa, alisema jambo hili ni zuri kwani linawapa mwanga wa kujiandaa wastaafu watarajiwa wa Mfuko. Pia alizipongeza taasisi mbalimbali zilizotoa elimu katika mafunzo hayo.

Akizunguza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Kaimu Mkurugenzi wa PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa alisema, jukumu la Mfuko ni  kutoa elimu kwa umma katika maeneo ya msingi, kama vile; Uanachama na Michango, Mafao na mambo muhimu yakuzingatia   katika ajira, wakati wa kustaafu na baada ya kustaafu.

Kaimu Mkurugezi Mkuu PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa akizumgumza katika semina kwa ajili ya Wanachama wa PSSSF mkoani Dodoma

Katika kuhakikisha wanachama wetu wanapata mafunzo ya uhakika katika uwekezaji, tumewaalika wenzetu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) ili kuwapatia ujuzi Wastaafu wetu watarajiwa, ili waweze kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo na hatimaye kutengeneza ajira kwa vijana wetu” alifafanua Bw. Magawa.

Wastaafu watarajiwa wa PSSSF wakifatilia semina waliyoandaliwa na PSSSF jijini Dodoma

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema, mpango huo wa semina ni endelevu ambao utaendeshwa kila mwaka kwa wanachama wa PSSSF waliobakiza kipindi kisichozidi miaka miwili kabla ya kustaafu. Semina hiyo iliendeshwa na PSSSF kwa kushirikiana na TBP, NMB, NBC, CRBD, DCB, SIDO, TAKUKURU, TCRA,  BENKI YA AZANIA, MCB na UTT AMIS.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.