Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi aendelea na ziara yake Wilaya ya kati Unguja leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi   alipokuwa akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya Kiboje Manzese kuzungumza na Wananchi wa Jimbo la Uzini leo mara baada ya kutembelea Barabara ya Kiboje,Miwani-Kizimbani akiendelea na  ziara  yake katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa huo.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili  na Mifugo Mhe. Sudi Nahoda akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kilimo kwa Wananchi na Wakulima wa Kiboje,Miwani-Kizimbani wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  (hayupo pichani)  alipotembelea Barabara ya vijiji hivyo vya Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo akiendelea na  ziara  yake ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa huo.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  (wa tatu kulia)  alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Mgeni Haji  Jimbo la Uzini   baada ya kutembelea  Barabara ya Mgeni Haji –Kwambani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja  akiendelea na  ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa huo leo.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  (kushoto) alipokuwa akimsikiliza Mhandisi Mansour Mohamed Kassim (wan ne kulia) alipofika kuangalia maendeleo ya  Mradi wa  ujenzi wa Hospitali ya Binguni Wilaya ya Kati akiendelea na Ziara  yake  kuangalia  maendeleo  ya  miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  (kushoto) alipokuwa akimsikiliza Mhandisi wa Idara ya Umwagiliaji maji Jogha Salum Mohamed (kulia)   alipofika kuangalia maendeleo ya   Mradi wa  kilimo cha umwagiliaji Bonde la Cheju  Wilaya ya Kati     akiwa katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali Mkoa wa  Kusini Unguja leo.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi   (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mzee Omar Iddi Omar Mkulima katika Bonde la Mpunga la Cheju  Wilaya ya Kati kuhjusiana na ukukulima wa mpunga katika Bonde hilo akiendelea  na ziara yake ya  kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja leo.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi   alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Abdalla Khatib Hamad katika kikundi cha wajasiria mali Mwera   alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Tunguu Suza  Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika ziara ya  Mkoa huo.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  (kulia) alipokuwa akimsikiliza Nd. Salum Mohamed Salum wa Ushirika wa Vijana ZAN MIX  wa Dungabweni  Wilaya ya Kati alipokuwa akitembelea maonesho ya Wajasiriamali wa Wilaya ya Kati Leo viwanja wa Ukumbi wa Tunguu Suza akiwa katika Ziara yake  katika Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Iklulu] 04Julai 2021.


Rais akihutubia katika Majumuisho ya Ziara Mkoa Kusini ukumbi Tunguu Suza Wilaya Kati Leo.[Picha Ikulu] 04Julai 2021
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.