Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe.Jamal Kassim Ali, amewateua wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar imesema, kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 7(2), (c), (i), (ii), (iii) cha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Namba. 2 ya mwaka 2005, amewateua wafutao.
1. Bw.Arafat Ally Haji
2. Bw.Assaa Sharif Khalid
3. Bw. Jaha Haji Khamis
4. Bi.Khadija Shamte Mzee
5. Bi. Sabra Omar Hussein
6. Bw.Said Abdalla Basleym.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 20, July, 2021.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO
No comments:
Post a Comment