Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia) akikabidhiwa kompyuta na Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) (aliyevaa barakoa) wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange wakikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Shule ya Sekondari Dutwa anayepokea ni Mwalimu wa shule hiyo Mekrina Bonifasi.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (mwenye miwani), akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkololo alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajili ya shule hiyo
Baadhi ya wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Nkololo wakifurahia ugeni uliofika shuleni hapo
ukiongozwa na Mbunge wa Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (hayupo pichani) kwa ajili ya kukabidhi vifaa
vya TEHAMA kwa ajili ya shule hiyo ambavyo ni printa 1 na Kompyuta 5
Na Faraja Mpina, SIMIYU
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya Shule ya Sekondari Dutwa na Shule ya Sekondari Nkololo zilizopo katika Wilaya ya Bariadi ambavyo ni kompyuta 10 na printa 2 ambapo kila shule imepatiwa kompyuta 5 na pinta 1
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Mbunge wa Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew ambaye ndiye aliyevikabidhi katika shule hizo akiambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Lupakisyo Kapange
“TEHAMA inaenda kuchangia kukuza uchumi wa dunia na sisi Tanzania tumeona kwamba tusibaki nyuma katika kukuza matumizi ya TEHAMA kwa kuhakikisha vijana wetu wanajifunza TEHAMA kuanzia shuleni na nikiwa kama Mbunge wa Bariadi nina kila sababu ya kuwasisitiza vijana wetu kusoma kwa bidii”, amezungumza Mhandisi Kundo
Naibu Waziri huyo ametoa rai kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kupata ufaulu mzuri katika mitihani yao ya Kitaifa na kusisitiza kuwa wanafunzi watakaopata ufualu wa daraja la kwanza la pointi 7,8,9 atawalipia ada kama alivyoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka 2020
Ameongeza kuwa mpaka sasa amekwishawalipia ada wanafunzi 18 wa kidato cha tano ambao wamepata ufaulu huo katika matokeo ya mwaka huu na wale ambao wamefaulu lakini familia zao zimethibitishwa kuwa hazina uwezo wa kuwaendeleza
Kwa Upande wa Mkuu wa Uendeshaji wa UCSAF Eng. Albert Richard amesema moja ya majukumu yanayotekelezwa na Mfuko huo ni kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma ili kuendelea kuinua matumizi ya TEHAMA nchini
Naye Mwalimu Mekrina Bonifasi wa Shule ya Sekondari Dutwa amesema kuwa msaada huo wa kompyuta utakuwa chachu ya ufaulu na utasaidia sana katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi hasa ukizangatia kuwa kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza wapatao 280 ambao wanasoma somo la kompyuta na watafanya mtihani wa Taifa 2022 kwa mara ya kwanza
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ambaye pia ndiye Mbunge wa Bariadi amesikitishwa na uongozi mzima wa Kata ya Nkololo kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa maabara ya TEHAMA katika shule ya Sekondari Nkololo wakati tayari Mbunge huyo alikwishapeleka mifuko 156 ya simenti na mabati 50 toka mwezi Machi, 2020 lakini mpaka sasa hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya kufyatua tofali 1500
Ameongeza kuwa, mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuja kuulizwa kimetekeleza nini wakati jitihada zinafanyika za kuleta nyenzo za kutekeleza yale ambayo yameandikwa kwenye Ilani ya Chama hicho ambayo ndani yake imeongelea masuala ya TEHAMA lakini bado viongozi wa Chama na Serikali katika ngazi ya Kata hiyo wameshindwa kusimamia utekelezaji wa yale yaliyokusudiwa
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Lupakisyo Kapange amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri na Wataalam wake wahakikishe wanatoka ofisini na kwenda kuweka kambi katika shule hiyo ili kusimamia ujenzi wa darasa hilo hadi ukamilike
“Baada ya hapa nataka nipate maelezo kwanini darasa halijakamilika kutoka mwezi Machi mpaka sasa na wakati vifaa vyote vipo, nani alikuwa anasimamia, nani alipinga na nani alichelewesha na taarifa hiyo niipate ndani ya wiki moja” alizungumza Mhe. Kapange
Aidha, iliamuliwa kuwa vifaa vya TEHAMA vilivyopelekwa kwa ajili ya Shule ya Sekondari Nkololo vihifadhiwe na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mpaka hapo chumba cha maabara ya TEHAMA ya shule hiyo kitakapokamilika ndio
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
No comments:
Post a Comment