Habari za Punde

Walimu Wakuu Wastafu wa Skuli za Wilaya ya Wete Pemba Waagwa.

MBUNGE wa Viti Maalumu Wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Asiya Sharif Omar, akizungumza katika hafla ya maagano ya walimu wakuu waliomaliza muda wao wa utumishi serikalini , hafala iliyofanyika katika kituo cha walimu Mitiulaya Wete.
MBUNGE wa Viti maalumu Wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, akimkabidhi zawadi kwa Mwalimu Mstaafu Bi.Ramla Omar Saleh, ambae amemaliza Utumishi wake serikalini wakati wa hafla ya maagano iliyofanyika katika kituo cha walimu Mitiulaya Wete
AFISA Mdhamini Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Pemba Mohamed Nassor Salim, akimtolewa wasifu wake juu ya ufanyaji kazi bora na kuhamasisha jamii juu ya suala zima la usafi wa mazingira Kojani, mwalimu Msaatafu Bakari Issa Omar kutoka Kisiwa cha Kojani, wakati wa hafla ya maagano iliyofanyika katika kituo cha walimu Mitiulaya Wete

BAADHI ya walimu wakuu wa Skuli za Wilaya ya Wete, wakifuatilia kwa makini hafla ya maagano ya walimu wakuu waliomaliza muda wao wa utumishi Serikalini, hafla iliyofanyika ukumbi wa Walimu Mitiulaya.

#(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.